McLaren W1 Supercar yazinduliwa. Ndio itawarithi McLaren P1 na F1. Itauzwa Billion 5.7 za Kitanzania tu!

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
26,927
77,688
McLaren Automotive jana tarehe 06 October wametangaza chuma yao mpya McLaren W1 wameipa codename P18.
IMG_0275.jpeg

Hii Plugin-hybrid itaanza kuuzwa mwakani 2025 na ndio itakayowarithi wakongwe P1 na F1 waliokuwepo tokea miaka ya 90s (F1) na miaka ya 2010s (P1).
IMG_0274.jpeg

W1 ni 2-doors coupé itakayokuja na gull-wing doors.
IMG_0277.jpeg

McLaren W1 ina 4.0L twin-turbo V8 hybrid engine inayotoa 928 hp, na 8 speed dual clutch transmission yenye electric reverse.
IMG_0276.jpeg

Hadi sasa, W1 ndio McLaren yenye acceleration kubwa kuwahi kuundwa, na inaenda 0-100 km/h ndani ya 2.7 seconds na 0-200km/h ndani ya 5.8 sec. Pia top speed inasemekana kua 350 km/h.
IMG_0279.jpeg

Bei ya W1 itakua approximately Billion 5.7 za Kitanzania na zitatengenezwa jumla ya gari 399 tu.
 
Kuna gari limited edition unakuta zinatengenezwa 10 tu Dunia nzima na baada ya hapo hawaruhusiwi kutengeneza zingine, 400 nyingi sana
Mnakua na group lenu la WhatsApp. Unajua mfano Ferrari ukitaka kununua gari lao jipya ni lazima uwe ushawahi kumiliki used Ferrari kwanza.

Na kuna baadhi ya model kama LaFerrari ili uinunue lazima uwe umeshawahi kununua Ferrari nyingine mpya kabla.

Tutafute hela.
 
Back
Top Bottom