Mchungaji Richard Hananja: Ni vizuri pia tukaangalia 'Super Baba', vijana wakiume wameachwa

informer 06

Member
May 11, 2024
63
46
Mchungaji Richard Hananja ametoa wito kwa walimu, wazazi na walezi na jamii kuwalea watoto katika malezi ya kuwaeleza ukweli ambao unaweza kuwaepusha na vitendo mbalimbali ambavyo havifai katika jamii.

Anadai kuwa watoto wa kiume wamekuwa wakiachwa nyuma hivyo amesisitiza umuhimu wa kuwazingatia katika malezi, huku akitolea mfano wa vitendo vya vinavyoenda kinyume na maadili mbavyo amedai kuwa ni changamoto inayoikuba jamii kwa sasa.

Ameyasema hayo Julai 27, 2024 kwenye mahafari ya wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Nuru Njema iliyopo Tegeta Jiji Dar es salaam wanaotarajiwa kuhitimu kwa siku za karibuni.

"Wachunge sana vijana wa kiume tuwaeleze mambo ya ushoga, usagaji na ulawiti bila kung'ata maneno"amesema

Alichozungumza mgeni rasmi Mkurugenzi Mkuu wa TET
img_5354-jpeg.3056264

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba amesema kuwa Serikali imefanya maboresho kwenye mitaala ya elimu ili kuwawezesha wahitimu kuwa na elimu ujuzi.

"Lengo kuu la maboresho hayo ni kuhakikisha tunatoa elimu ujuzi"amesema , Dkt.Aneth

Akizungumza katika maadhimisho hayo Dkt.Aneth amesema kuwa maboresho yaliyofanyika ni ya sita tokea uhuru, ambapo ametaja tija zake kuwa ni pamoja na kulenga kukuza ubunifu, fikra tunduizi, mahusiano na kuonesha mwelekeo wa ajira.

Amengoza kuwa katika mchakato wa kuandaa mitaala hiyo zilifanyika tafiti ili kujua mahitaji ya wananchi kujua wananchi wanataka nini na wanataka elimu ya aina gani.

Ambapo amedai kuwa kati ya mambo ambayo waligundua ni kwamba umma ulikuwa ukiitaji elimu ya ujasiliamali. Amedai kwamba kufuatia hitaji hilo waliamua kuchakata maoni na kuamua kuja na somo la elimu ya biashara linalenga kujumuisha masuala mbalimbali yatakayomsaidia muhitimu kuwa na ujuzi katika masuala ya kibiashara.

Hata hivyo ametoa wito kwa wazazi na walezi kushiriki vyema katika utekelejazi wa mtaala huo kwa kuwafundisha watoto stadi mbalimbali ambazo zinawajenga kuwa na uwezo wa kufanya kazi, wito wa aina hiyo pia ameutoa kwa shule kuendelea kutoa elimu ujuzi na kuwapa muda wanafunzi kushiriki katika masuala ya kimichezo.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shule za Nuru Njema amesema wanazingatia vyema mitaala ya Serikali kwa vitendo, jambo ambalo amedai limekuwa likipelekea shule zao kufanya vizuri katika mitihani.

IMG_5485.jpeg

Mkurugenzi wa Shule za Nuru Njema

Lakini kufuatia uwepo wa taarifa mbalimbali za madai kuhusu baadhi ya watoto kutekwa katika maeneo tofauti nchini, amesema kuwa shule hiyo imekuwa na utaratibu rafiki ambao unasaidia kuweka watoto katika mazingira salama.

Amesema kuwa kwa sasa katika Shule hiyo Wanafunzi hususani wadogo lazima wachukuliwe na watu wanaotambulika kwa uthibitisho.
 

Attachments

  • IMG_5354.jpeg
    IMG_5354.jpeg
    1.9 MB · Views: 15
Back
Top Bottom