Kuelekea 2025 Mchungaji Msigwa kwenda CCM ni moja kati ya 'usajili' mbaya kuwahi kufanywa na vyama vya siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Jan 9, 2022
1,289
2,825
Kwa sasa Tundu Lissu ndiye mwanasiasa pekee ambae kuhama kwake sehemu kunaweza hama na watu , sababu nyuma kuna watu wengi sana ambao ni wafuasi wake na wana imani na yeye.

CCM wamemchukua Msigwa kama mtaji ndio maana anapewa airtime kwenye mikutano.

Kiuhalisia sasa ni kwamba Mchungaji imani na mvuto kwa wana CDM ulishapotea hata ushindani uliotokea kwenye uchaguzi wa kanda ni kwa wajumbe wanakosa mtu mwingine sahihi katika hiyo nafasi ila wote ni wabovu.

Lakini pia ni bad timing sababu 1. Unapokea mtu tayari ameshindwa uchaguzi kwanini hakuhamia kabla ya Uchaguzi wa kanda?

2. Msigwa ilibidi apokelewe CCM kama mwanachama wa kawaida halafu aanze kupewa time jukwaani taaratibu hasa kuelekea 2025 - sasa watu wanamchulia kama msaliti fulani na mroho wa Madaraka.

Kwangu mimi huu ni usajili mbovu kuwahi kufanywa na vyama.

Soma Pia:

- Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM


- Kuelekea 2025 - Yaliyojiri kwenye mahojiano kati ya Chief Odemba na Peter Msigwa kwenye kipindi cha Medani za Siasa
 
Uko sahihi tena ameanza siasa za kujisafisha mapema na kukashifu alikotoka, (castigation), na hili limetokea muda mfupi baada ya kushindwa uchaguzi wa uwenyekiti wa kanda ya nyasa wa chama cha chadema.

Mimi kuna tatizo nimeligundua linalo tokana na tabia ya wanaopewa dhamana ya kuongoza tabia hii ni ya kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi a.k.a kujizima data, hii tabia kwasasa imejinga miongoni mwetu eti baadhi ya watu wameamua kuishi nayo matokeo yake wakiwa majukwaani hushindwa kujenga hoja, hii tabia nimeipa jina la unyumbu
 
Kwa sasa Tundu lissu ndiye mwanasiasa pekee ambae kuhama kwake sehemu kunaweza hama na watu , sababu nyuma kuna watu wengi sana ambao ni wafuasi wake na wana imani na yeye .​
Mkuu Nehemia Kilave , wewe utakuwa huwajui Watanzania!. Kuna mtu alikuwa na mvuto na wafuasi kama Lowassa ile 20l5?, alipohama CCM kujiunga Chadema alishobokewa sana kuwa atacama na mtaji wake wa watu, hata mimi niliamini hivyo Elections 2015 - Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio! kilichokuja kutokea ni Lowassa alihama peke yake!. Hata Lissu leo akiamua kuhamia ACT Wazalendo, utashangaa!, atahama yeye peke yake!. Kwenye siasa zetu, hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu kuna maslahi tuu ya pomoja and no one is indispensable!.
P
 
Umetumia lugha safi sana na yakiungwana kuelezea hili ila huyu mchungaji feki hastahili kuheshimiwa...yeye na yule KAHABA NI WAPUMBAVU NA NI WASHENZI...HAWATAKIWI KUAMINIWA POPOTE PALE.
 
Ni vyema kutoa mtazamo wako na hisia zako je nchimbi na samia wana maoni gani?
 
Ni kweli EL alihama na watu ingawa wengine waliendelea kimwili kuvaa kijani hili liko wazi P
 
At least leo umeongea vizuri Kidogo, twende ibadani.
 
Kwa sasa Tundu lissu ndiye mwanasiasa pekee ambae kuhama kwake sehemu kunaweza hama na watu , sababu nyuma kuna watu wengi sana ambao ni wafuasi wake na wana imani na yeye .📌🔨
 
Lissu hivi karibuni alisema kuwa CCM imejaa viongozi wasio na akili, CCM yenyewe inathibitisha kwani imeshindwa kumuuliza Msigwa wale wafuasi wake 200 aliowaahidi wako wapi badala yake wanatangatanga naye kama walozi.
 
CHADEMA tujifunze ku-move on.
Tukubali kwamba Siasa ndio ajira ya MwanaSiasa. Imejengeka tabia ya Kichawi, Kishamba na isiyo ya Kisomi kumuona mtu anayehama CHADEMA kama hafai, garasa nk. Mwishowe sisi tunaoendekeza tabia hizi ndio hamnazo.

Tujifunze kuziishi siasa zetu, tujifunze kwamba Chama alichopo Mwanasiasa siyo baba yake na Mama yake kesho au leo anaweza kuondoka! Na akiondoka achana naye.

Mnakuwa na akili ndogo na finyu kama WanaYanga vs FEI TOTO! Badilikeni Makamanda muache kulia lia na kurusha Vijembe kama waimba Taarabu.
 
Nehemia Kilave ninakuita Ndugu yangu
Nadhani kuna namna fulani dhana ya Siasa kidogo huijui.

Kwanza kabisa Chama cha Siasa huwa kinajenga Ideology ambayo huwa inaaminiwa na wafuasi wake. Kama zilivyo dini, siasa nazo ni mfumo wa namna hiyo.

Mchungaji Msigwa siyo lengo pekee la kuongeza wafuasi ndani ya CCM bali pia kuongeza wigo wa watu wanaosikiliza sera za CCM.

Kumbuka mpaka sasa kunahoja ambazo Msigwa amezitoa ambazo zimezalisha attention kwenye Taifa. Hata wale waliokuwa hawamfuatilii MSigwa kila mkutano akienda watataka wasikie anaongea nini..

CCM haihitaji watu wote ndani ya CHADEMA bali inahiaji baadhi ya waliomo ndani ya Chama hicho wanaomuunga mkono Msingwa.

CCM tayari ipo na wanachama Hai zaidi ya 15,000,000.
 
Maoni yako binafsi yaheshimiwe,sisi wengine tunaona ni usajili bora kabisa kuwahi kutokea, na kazi yake kuu kwa sababu alikuwa chumbani anajua Siri zote za hiyo Sacco's yenu, ni kuwafirimba tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…