Mchezo wa mpira wa miguu na uchumi

conductor

JF-Expert Member
May 29, 2013
798
660
"Mungu ni wetu sote" , Nitakwenda na mfano wa nchi ya KOREA,(huko nyumba miaka 1961), wakati Tanzania inapata Uhuru, tulikuwa mbele Yao (kiuchumi)katika kusafirisha nje malighafi, lakini pia hawakuwa na cha kusafirisha nje ya nchi Yao, ndo kipindi Hicho Hicho wakapata nguvu ya kufikiri namna yakujikomboa kiuchumi.

Mtaji mkubwa walikuwa nao, ikabidi wabuni vizuri kupitia ushawishi wa mabinti zao kuwa na nywele nzuri na ndefu, ikabidi wazifanye malighafi ya kuuza nywele za mabinti zao nje (waliwanyoa na kuzipaki vizuri na kuuza nje Kama wigi), ndo Pesa yakigeni walivyoweza kuipata, (hili ni kiwango cha juu kabisa cha kufikiri cha wakorea wakati huo na nawapongeza Kwa kubuni malighafi ya nywele), hata hivyo Leo hii bado Kwa uhaba wa ardh bado wakawekeza kwenye technolojia Leo hii Samsung na vifaa VINGI vya kielectroni wanauza wao DUNIANI, sasa leo NCHI nyingi dunian wamewatangulia Sana.(mfano huu unatusaidia kuacha kulaumu Bali tuwe wabunifu Kama nchi na Kama wahanga wa uchumi kuwa ngumu na Ajira na mitaji).

No.2, Wakati KENYA kwenye mashindano ya Olympics wanakwenda na michezo tofauti takriban 28, Tanzania bado tunatumia mfumo unaitwa TRADITIONAL GAME( iko Kama 9 hivi) , kiasi kwamba hata ndege inayobeba wachezaji inapata faida "seat capacity" inayostahili kuliko Tanzania (9:28),bila Shaka hata wewe ungependa uanzishe route ya Kenya kuliko TZ,(damand pull),USA INA zaid ya michezo 2000, hivyo unaweza kuona ni vipi Tz INA NAFASI kubwa kutumia kuchelea kwake kuona fursa wakanakiri (copy) Kwa wenzentu, Wakati Kenya INA Maprofesor 5000, Tanzania sijuhi Kama wanafika 3000, hii kitaalum inaitwa (gape between)

Mifano hiyo juu inalenga kukufungua bongo zetu kuwa KUPATA PESA YA KIGENI itakuwa ngumu Sana ili kukwamua Maisha yetu kwani HaKUNA tulipo wabobezi wala wabunifu kuwazidi wenzetu.

Wakati WA KOMBE LA DUNIA (2022)nchini Qatar, nchi ya MOROCO (MAROCO) ilijizolea umaarufu mkubwa kufika robo fainali ya mashindano hayo ya FIFA na kukukiri kuwa pia WALIWEKEZA PESA katika VIJANA kupitia Academy ambayo hata hiyo iliwapatia Pesa zakigeni zaidi ya DOLA 20M, Jambo hili linaweza kuwa kichocheo cha TZ kuona ni njia ipi itatumia kuwainua Vijana na wataalam wake kujipatia kipato, Nimekutana na Manager wa FOUNTAIN GATE ya DODOMA (huko USA) akifanya utafiti namna gani wengine wamefanikisha kutoka shule za mpira wa watoto(football academy),ili waboreshe Fountain gate sport club Yao, nilipomuuliza swali NAFASI YA Fauntain gate sport nchini Tz, alinijibu kuwa zaidi ya wachezaji 8 wa kike walishiriki kombe LA DUNIA la wanawake nchi INDIA 2022, wakifuatiwa na SIMBA, (hivyo wao walitoa wachezaji zaidi) kwangu nilioona Kama Mwanga nzuri katika michezo,Ila nilipomuuliza CHANGAOMOTO alijibu hawako tayri kukata tamaa, licha ya Watanzania wengi kutokuwa na MWAMKO WA MICHEZO na uwekezaji.(Alikwepa kumpa lawama MTU yeyote zaidi ya kusema elimu ya ubunifu ndo shida kubwa).

Nilivyokutana na mchezaji wa zamani na Mwalimu wa Academy (PASS ACADEMY)iliyoko USA, katika mashindano ya michezo ya team ya BRAZIL NA COLOMBIA katika michuano ya 5v5 (Futbol de salon)iliyoko Chini ya IFFS, Mr.ALEX KAJUMULO, ambae ni MTANZANIA anayeishi USA, nakufanya KAZI pia CANADA ,nilimuuliza Tanzania nchi yako iko wapi katika USO WA MICHEZO DUNIANI hususani MPIRA, alinijibu TANZANIA wanapenda Team hawapendi MICHEZO, ndo maana SIMBA NA YANGA zinapendwa kuliko Vilabu vingine, lakina akaongeza Kwa kusema tangu 2020, nilianza kuleta ushawishi na elimu yangu ya mpira kutoka nchi zaidi ya 108 nilizotembelea kujifunza na kufanya biashara ya michezo kuona Kama TANZANIA itaweza kufufuka kwenye Michezo,Ila KAZI kubwa inayoitajika TANZANIA nikuwekeza katika Watoto na Kwa kufungua academy nyingi, lakini pia kushirikiana na nchi zilizondelea kufanya joint venture kwani TANZANIA INA vipaji VINGI na hali ya hewa ya Tanzania inaushirikiano (air density)kupata vijana WAZURI kucheza vilabu vikubwa, ila anamini katika kufundishia hata Kama unakipaji vipi , lazma upate makocha,walimu,marefaree,vitabu,viwanja vizuri, vifaa vya michezo na msukumo wa serikali katika kuboresha mazingira ya watoto na vijana kucheza, akaongeza Kwa kusema licha ya Michezo ni Afya Ila serikali unaweza kutenga bajet ya kuboresha hospital ambapo mgonjwa MWISHO WA siku watamwambia fanya mazoezi, lakin huwez kuta bajet ya viwanja,shule za michezo au bajeti ya kujenga chuo kikiuu cha michezo Bali michezo inachukuliwa Kama BONANZA, katika ulimwengu wa leo lazma "specialization" ipewe NAFASI.

Nilipotembelea CHUO cha MICHEZO MALYA_KWIMBA huko mwanza, nikakutana na wanafunzi wanasoma cheti na diploma ya michezo chuoni hapo CHANGAOMOTO Yao kubwa walioonyesha NI bajeti ndogo wanayopata katika kuendesha chuo, kiasi kwamba hata wanafunzi hawana vitendea KAZI kuweza kuzalisha wachezaji na walimu WAZURI, nilipowauliza je kuna Team ya chuo ambayo inashiriki mashindano yoyote hapa nchini na daraja gani, nilijibiwa kuwa tunatafuta wakuwadhamini kuboresha hata viwanja vya chuoni hapo, nilipowauliza field zenu za michezo mmewahi kuifanyia nje ya nchi ili kujifunza zaidi walioonyesha kushangazwa na swali Hilo, je kuna academy hapa shule hapana, ,nikatembelea CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAM, idara ya Viungo na MICHEZO kuona Kama kuna DIRA yoyote ya kubuni na kuboresha WASOMI wanaohitimu hapo na Kama Wana viwanja vya kutosha mkuu WA idara ya michezo alionyesha bajeti ndo CHANGAOMOTO lakini pia wanakaribishwa ANDIKO (PROPOSAL) kuboresha Michezo na kuandika vitabu vya michezo, (DR TIBOLOHA).

Nikakutana na Boss wa BMT wako huo DR SINGO (BARAZA LA MICHEZO TANZANIA),vipi DIRA ya michezo Kwa Tanzania je inachingia uchumi WA nchi inavyotakikana, alinijibu kuwa DIRA nikupanua wigo WA kuwa na michezo mingi zaidi ili kupata NAFASI YA kushiriki mashindano Mengi yatakayo panua uzoefu wa vijana na team zetu, nilipo uliza Kama ratio ya mapato ya michezo (market share) nchini Tanzania alisema tunataka kutoka kwenye TRADITIONAL competition to Innovation games na hiyo itachangia Sana kuongeza Ajira na kuongeza kipato Kwa nchi, Nikatembelea Mbeya (Tulia trust) hawa ni wadau wakubwa wa kusaidia vijana na kuibua vipaji vya michezo lakini pia kusaidia vijana, nikakutana na mwanariadha wa ZAMAN Mr Morris ukimsikiliza vizuri utagundua industry ya kukimbia analijua vizuri na alifanya vizuri katika nyakati zake, nilipo muuliza Kama kuna vijana wakufuata nyayo zake pamoja na wakina Ikangaa,Bayi alisema TZ inaitaji watu wenye moyo na nia ila vipaji vipo vyakutosha Ila hata viwanja changa Moto, Kiwanja cha kukimbilia,ndo Hicho cha mpira wa MIGUU,ndo Hicho cha mikutano ya hadhara,ndo Hicho cha Mwenge nk, pia huwez kwenda bank kuombea mkopo ili ujengee uwezo vijana (hudhaminiki),hata hivyo maombi ya vijana kuomba sponsorship ni wengi kila sekta ya MICHEZO.

Nikatembelea Kampuni ya SBS (ndani yake ndo kuna PEPS)wazalishaji na wauzaji wa vinywaji barid nchini TANZANIA,nikakutana na mdau mkubwa Sana wa MICHEZO Mr.Deo KWAY nikamuuliza Kama peps inayoajiri vijana wengi kuzalisha kinywaji pendwa Kama ina team inadhaminiwa na PEPS je kuna MWAMKO WA kimashindano alinijibu kitaalamu kabisa kuwa team IPO ya PEPS Ila sio team ya kampuni Bali NI michango ya wafanyakaz wa PEPS Kwa mapenzi binafs kiasi kwamba huwa wanjichanga wakati mwingine kupeleka team uwanjani, Kampuni inatia michango mdogo usiokidhi hata mahitaji ya team kwenda uwanjani, Nilipomuuliza Kama PEPS kwanin i haibeb mzigo huo kitaalam Kama (re energising to workers)ukizingatia wachezaji wa team nyingi wanakunywa soda na maji hivyo kuna haja ya kutenga bajeti yake alisema Wazo kubwa walilonalo ni kuzidi kujichanga kama wapenz wa Mpira kutengeneza team kwani PEPS mpira sio kipaumbele kikubwa, wao kuzalisha kinywaji, nikaona nionane na Kiongoz mkubwa mwenye asiri ya INDIA (MARKETING DIRECTOR) anajulikana Kama JITEN, nilipomuuliza DIRA yakusaidia michezo hususani team ya PEPS Kwa asilimia 100 na kusaidia vijana na kujitangaza ,aliniuliza Kama Mimi ni MTANZANIA au natokeq nchi jirani, hivyo akakunja na Sura ya kuboreka na swali Hilo, hivyo nikapata JIBU kuwa Njia kukomboa nchi kupitia MICHEZO inaitaji pressure iliyokubwa kuliko iliyozoeleka (ADIABATIC PRESSURE)

Kutokana na UTAFITI WANGU MDOGO huo nikagundua hii NI "forgotten opportunity" Kwa nchi na watu wake, kiasi kwamba inaitajika juhudi na ubunifu wa khali ya juu kutumia MICHEZO Kama kitega uchumi na fursa kubwa zaidi Kwa nchi, hatuwez kufikiri UTALII,AFYA,ELIMU,ukaacha MICHEZO ambayo inahitaji promotion kuleta Pesa mpya nchini.

Leo hii CR7 (Ronaldo) kitendo Tu cha kujiuga na Team kutoka nchi ya Saud Arabia, team imeongeza watazamaji kutoka 860 mpaka milion Kumi kupitia mitandao ya kijamii histagram, hivyo Kwa lugha ya kawaida Sana ya uchumi waliofungua gugo Saudi Arabia ni Sawa na kuchangia pato la Taifa (online business) kutoka 860 Mpaka 10m, sasa kila MTU ajiulize alilipia currency ipi kusearch hiyo team na nchi. Tutafakari PAMOJA KUHUSU MICHEZO na Nguvu ya MICHEZO.aksante Sana.

FB_IMG_1672698102244.jpg
image_f44788c7-0d99-467e-98fc-ff816502a50720230102_221658.jpg
 
Asante sana kwa andiko umegusa penyewe,japo muandiko wako changamoto..ubarikiwe
 
Asante sana kwa andiko umegusa penyewe,japo muandiko wako changamoto..ubarikiwe
Nimeandika MICHEZO na UCHUMI moderator akabadiri title. Nashauri ama afute article yote au arudishe title yangu. (Uko ni kuingilia idea yangu) hiyo sio linguistics.
 
Nimeandika MICHEZO na UCHUMI moderator akabadiri title. Nashauri ama afute article yote au arudishe title yangu. (Uko ni kuingilia idea yangu) hiyo sio linguistics.
Naunga mkono mkuu, hao vilaza waache ujuaje wakati ni empty
 
Back
Top Bottom