TANZIA Mchezaji Beno Kakolanya afiwa na Mama yake

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,107
5,049
Kipa wa Simba, Beno Kakolanya leo Agosti 19, 2021 asubuhi amefiwa na mama yake mzazi anayeitwa Eva Mwankusye na msiba upo kwao Isyesye jijini Mbeya.

Taarifa za msiba huo zimethibitishwa na kaka wa mchezaji huyo, Asajile Mwakalindile ambaye alikuwa na mama huyo muda wote.

Mwakalindile amesema; ”Ni kweli mama amefariki leo asubuhi na bado tupo hospitali,”

Mke wa Kakolanya anayefahamika kwa jina la Hadra, aliliambia Mwanaspoti mama mkwe wake ni kweli amefariki na anamsubiri mumewe arejee ili waweze kusafiri kwenda Mbeya.

Kakolanya yupo nchini Moroccco na kikosi cha Simba katika maandalizi ya msimu mpya lakini anatarajia kurejea nchini kesho kwa ajili ya mazishi kwa ajili ya mazishi ya mama yake.

Chanzo: Mwanaspoti
 
Pole nyingi kwa Kakolanya na familia nzima kwa ujumla! Mwenyezi Mungu ampunzishe pahala peponi Amina!
 
Back
Top Bottom