''Mchepuko'' ulivyotaka kuharibu shughuli ya msiba wa muimbaji wa nyimbo za injili Marco wa Zabron Singers

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
20,248
49,904
Kuna wanawake ni nusu watu nusu hayawani.

Takriban wiki moja iliyopita muimbaji wa nyimbo za injili Marco Zabron wa kundi la Zabron Singers alifariki jijini Dar es salaam.

Mapema wiki hii shughuli ya mazishi ikawa inafanyika huko Kahama mkoani Shinyanga kwao na marehemu.

Marehemu alikuwa ameoa na ana watoto.

Katikati ya majonzi msibani akaibuka huyu nusu mtu nini sijui na kudai yeye eti alikuwa mchepuko wa mtumishi amezaa nae na anataka mgawo wa mali au mtoto atambulike rasmi.

Mchepuko umekuja na kadi ya clinic, mawasiliano ya WhatsApp na picha walizopiga na marehemu kama ushahidi.

Yaani disco aliingia mmasai. Kwanini hakusubiri msiba ukaisha akaenda kistaarabu kujitambulisha.

Nimelia sana maana hata mi nikifa leo naweza kupata aibu kama hiyo na ninavyo heshimika kanisani.

 
Back
Top Bottom