Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,603
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa amewaelekeza wasimamizi wa vituo vya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwasaidia wapiga kura kusoma orodha ya majina vizuri ili wote waliojiandikisha wapate fursa ya kupiga kura.
Mchengerwa amesema hayo mara baada ya kupiga kura katika kituo chake alichojiandikishia cha Umwe Mchikichini kilichopo Ikwiriri Jimboni kwake Rufiji Mkoa wa Pwani.
Waziri Mchengerwa amesema taarifa alizonazo mpaka sasa ni kwamba uchaguzi unaendelea kwa hali ya amani na utulivu katika maeneo mbalimbali nchini.
PIA SOMA
- LGE2024 - Mchengerwa: Matokeo ya uchaguzi kutangazwa ndani ya saa 72