Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 30,681
- 34,080
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa ameeleza kuwa tuhuma zilizoibuliwa na Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo wakati wa mjadala wa bajeti ya wizara yake ni tuhuma za uongo na zisizokuwa na uthibitisho, akieleza kuwa hakuna fedha iliyopotea ama kuibiwa katika utekelezaji wa ujenzi wa jengo la Utawala la Halmashauri ya Arusha Jiji.
Soma Pia: Gambo aibua tuhuma za ufisadi wa mabilioni Arusha, Spika Tulia amwagiza Mchengerwa kuandaa ripoti iwasilishwe Bungeni
Mchengerwa amebainisha hayo mara baada ya kufuata maelekezo ya Spika Tulia Ackson aliyemtaka kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo zilizowasilishwa na Mhe. Gambo ambapo Mchengerwa ameeleza kuwa tuhuma hizo ni tuhuma zisizokuwa na mzizi, zisizokuwa na hoja, akiziita kama cheche za siasa ambazo hazifai ndani ya taasisi zenye misingi ya kisheria.