Mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa Taifa - Tanzania - Indaba

S. S. Phares

JF-Expert Member
Nov 27, 2006
2,138
84
Wadau,

Leo nimeweza kuhudhuria Mkutano wa Sekta za Madini, Nishati na Miundombinu Tanzania - Indaba, uliofanyika Ukumbi wa J.K. Nyerere Convention Centre. Mojawapo ya mada zilizotolewa na wadau wa Madini na Nishati ni hii: MCHANGO WA SEKTA YA MADINI KATIKA UCHUMI WA TAIFA. Mada hii ilitolewa na Mtendaji Mkuu wa TMAA, nimeiweka hapa jamvini ili wadau na Wananchi kwa ujumla muweze kujisomea na kuchangia maoni yenu.

Nawasilisha.
 
Attachments

  • TANZANIA INDABA 2013_TMAA.pdf
    2.4 MB · Views: 576
Nice presentation, imejaa takwimu muhimu zinazoonesha jinsi Serikali inavyofaidika na uchimbaji wa madini tofauti na wengi wanavyofikiria. Asante Mdau
 
Nice presentation, imejaa takwimu muhimu zinazoonesha jinsi Serikali inavyofaidika na uchimbaji wa madini tofauti na wengi wanavyofikiria. Asante Mdau

Na kweli serikali inafaidika! Zikitoka serikalini zinaenda kwa wabunge, baada ya wabunge ruzuku za vyama. Mwananchi anaambulia makombo. Lakini kuna siku Mungu anayeishi atawaadhibu.
 
Na kweli serikali inafaidika! Zikitoka serikalini zinaenda kwa wabunge, baada ya wabunge ruzuku za vyama. Mwananchi anaambulia makombo. Lakini kuna siku Mungu anayeishi atawaadhibu.
Kumbe sio haba, shilingi trilioni 1.7 kwamiaka kumi je tungetumia kujenga barabara yalami tungepata barabara yenye 1700km au madarasa bora 43000. Tmaa na serikali kwa ujumla kazeni buti ili tuendelee kuvuna kama nchi. Nimeipenda hiyo presentation imetulis
 
Mkuu tatizo sio makusanyo, mgawanyo wake ndio mgogoro: mbunge 11.2m/month, waziri 20m/month, ruzuku za vyama x1000CCM, x200cdm, x0.4cuf, zinawarudia watu walewale. Za kujengea barabara zitatoka wapi?
 
presentation imetulia. sema tungefanyia kazi hii report ya Fraser ili tuwezekuvutia zaidi wawekezaji kwasababu. tuna kila sababu ya kujipongea kwa nafasi tuliyonayo duniani. kunamaeneo mengine tumekuwa wapili duniani na kati ya nchi 25 duniani hatujashika hata nafasi ya 5 mkiani. kumbe tunaweza!! soma hapa
image.tiff

image.tiff

image.tiff

image.tiff
 
S. S. Phares, a-dot, JIS, Magurudumu,

..mnaweza kutuchanganulia makampuni[barrick, etc] ya madini yamechuma kiasi gani, na serikali imepata kiasi gani?

..je, tumepata 1.7trillion kila mwaka? au ktk miaka kumi tumepata 1.7 trillion?
 
Last edited by a moderator:
Kumbe sio haba, shilingi trilioni 1.7 kwamiaka kumi je tungetumia kujenga barabara yalami tungepata barabara yenye 1700km au madarasa bora 43000. Tmaa na serikali kwa ujumla kazeni buti ili tuendelee kuvuna kama nchi. Nimeipenda hiyo presentation imetulis

Duh!
Kweli wajinga ndio wakiwao, Yani 1.7 Tril kwa miaka 10 ? Alafu unasifia? Kweli hii nchi inaendeshwa na PAYE.
 
S. S. Phares, a-dot, JIS, Magurudumu,

..mnaweza kutuchanganulia makampuni[barrick, etc] ya madini yamechuma kiasi gani, na serikali imepata kiasi gani?

..je, tumepata 1.7trillion kila mwaka? au ktk miaka kumi tumepata 1.7 trillion?

Ndugu yangu hiyo ni kwa Miaka 10.
Umesahahu ule mkataba wa kumega Selou na kuchimba Uranium kwa Miaka 10 na wanasema watapata 200Mil USD na serekali itapata 5Mil USD kwa Mwaka. Sasa huoni Umangungo huu? Ya tunapewa 2.5% ya Mapato kwa mwaka kwa hesabu hiyo nadhani utakuwa ushajua kama tulipata 1.7 Tril then wao walipatA 68 Tril. Hivi hii ni Akili au Ujinga?
 
Last edited by a moderator:
Nilichojifunza kutokana na hii presentation, kwenye slide ya nne ni; hatuoni aibu wala kujihoji kwa nini tunatembea juu ya ardhi tajiri namna hii na bado tunakubali kuambiwa kuwa sisi ni maskini!

Pia nimependa ujumbe wa picha katika hitimisho la mada. Kwa tafsiri yangu ya haraka, japo waliotumika ni wazungu, lakini maana ni kwamba sisi tumegeuka kituko kiasi kwamba badala watu waende mbugani kuona na kuwashangaa wanyama, kinyume chake wanyama (simba) ndiyo wanatoka porini kuja kutushangaa Watanzania!
 
Back
Top Bottom