Mercenary2013

Senior Member
Dec 24, 2013
105
170
Salamu Wakuu Leo Napenda Kuwashirikisha Katika Mchanganuo Huu Wa Biashara Ya SALOON Hasa Ya Kiume.

Biashara ya SALOON Ya Kiume ni Wazo Zuri. Hapa chini Nimekuandalia Mchanganuo Wa Biashara Hii Pamoja Na Gharama Halisi (Makadirio) Za Kuanzisha Saluni ya Kiume.

KUMBUKA BEI/GHARAMA ZA VITU HAPA CHINI NI MAKADIRIO, HIVYO NI VEMA KUPATA GHARAMA HALISI KABLA YA KUANZA BIASHARA HII.

Tuache Stori Nyingi Twende Moja Kwa Moja Kwenye Mchanganuo Huu.

🔵KWANZA KABISA UNAPASWA KUELEWA VITU VIFUATAVYO KABLA YA KUANZA BIASHARA:

1. Ni Vema Kupata Eneo la Mjini au Sehemu yenye watu wengi ili kupata faida zaidi

2. Japo Saloon Ni Ya Kiume Ila Itabidi huduma iwafikie na Wanawake wa rika zote wenye kupendezwa na kunyoa mitindo huska.

3. Unaweza Pia Kutangaza Biashara Yako kupitia mabango, mitandao ya kijamii, na ofa maalum kwa wateja wapya.

GHARAMA YA VIFAA Mbalimbali VYA AWALI:


Viti vya KUNYOA (Virefu) 80,000 x 2 = 160,000

Benchi: 1 x 30,000 =30,000

Mashine za Kunyoa: TZS 80,000 x 2= TZS 160,000

Kabati Kubwa (Kuhifadhi): 1 x50,000 =50,000

Vioo Vikubwa: 1 x 150,000 = 150,000

Sterilizer Mashine: 1 x100,000 = 100,000

Mataulo Ya Kumfuta Mteja/Kukausha: 30,000

Picha Na Mapambo Ya Saloon: 30,000

Gharama za Leseni na Vibali: 80,000

Vifaa Vinginevyo (Vitana/Nyembe): 30,000

♂️Jumla Ya Gharama za Vifaa vya Awali: 820,000

✅ GHARAMA ZA UENDESHAJI NA MATUMIZI:


Gharama Ya Eneo (KODI Kwa Mwezi ): 50,000

Umeme Na Maji (MWEZI 1) = 50,000

Mafuta/Dawa Ya Nywele (Spirit): 50,000

Tahadhari Yoyote Kazini (MWEZI 1): 40,000

Mshahara wa MFANYAKAZI: Kijana Wa Kazi Atapaswa Kukusanya Hesabu Ya TAJIRI/MWAJIRI Ambayo Ni 30,000 Kwa Siku Itakayozidi Ndo Hesabu Ya Mfanyakazi. TAZAMA HESABU KAMILI HAPA CHINI

♂️Jumla Ya Gharama Za Uendeshaji: 190,000

✅MAPATO YA KUPATA KWA MWEZI:
(Hii Chukua Makadirio Ya Wateja 20 Kwa Gharama Ya 1,500 Kwa Kunyoa Kawaida Ukiachana Na Style Ambazo Itaongezeka Gharama)

Wateja kwa Siku: 20

Gharama Ya Kunyoa (Inategemea Na Eneo): 1,500

Mapato ya Kila Siku: 20 x 1,500 = 30,000

Mapato ya Kila Mwezi (SIKU 25): 25 x 30,000 = 750,000

✅FAIDA KWA MWEZI:
Mapato Ya Mwezi: 750,000

Gharama Za Uendeshaji: 190,000

Faida Ya Kila Mwezi: 560,000

✅ FAIDA KWA MWAKA (Miezi 12):

Mapato Ya Mwaka (Miezi 12): 12 x 750,000 = 9,000,000

Gharama Za Uendeshaji Kwa Mwaka: 12 x 190,000 = 2,280,000

♂️Faida Utakayopata Kwa Mwaka: 6,720,000/=

Kwa Mchanganuo Huu, Unaweza Kuona Kuwa Kuanzisha Saluni Ya Kiume Ni Biashara Yenye Faida Nzuri Ikiwa Itasimamiwa Vizuri.

KUMBUKA:
Haya Mahesabu Ya Kuingiza Kipato Kwa Siku Inategemeana Na Eneo Lako La Kazi, Biashara siku Zote Ni Kuandaa Mipango, Kuufanyia Kazi Pamoja Na Kuboresha Huduma Bora Zaidi Kwa Mteja.

ALL THE BEST WAKUU
 
Biashara za makaratasi zinavutia sana. Ila hapo hujataka kabisa ku consider business growth, kwamba kuna muda hautapata hata mteja mmoja kwa sababu bado biashara inakuwa. Wewe umewaza faida tu, haha
 
KUMBUKA:


Haya Mahesabu Ya Kuingiza Kipato Kwa Siku Inategemeana Na Eneo Lako La Kazi, Biashara siku Zote Ni Kuandaa Mipango, Kuufanyia Kazi Pamoja Na Kuboresha Huduma Bora Zaidi Kwa Mteja...
 
Na wasiwasi mkuu unaomba ushauri wa namna ya kuifanya hii biashara, maana hata hesabu zako hazijakaa sawa.
 
Mshahara wa MFANYAKAZI: Kijana Wa Kazi Atapaswa Kukusanya Hesabu Ya TAJIRI/MWAJIRI Ambayo Ni 30,000 Kwa Siku Itakayozidi Ndo Hesabu Ya Mfanyakazi. TAZAMA HESABU KAMILI HAPA CHINI
Vinyozi ni kama Madalali akili zao.

Unafungua Barbershop ya 5M anakwambia atakuwa anakulipa elfu 70 kwa wiki.

Hii biashara nimaachana nayo fremu ya Mtu nikaacha kulipa.
 
Mchanganuo uko vizuri sana na unaendana hasa na kitu nilichokifanya miaka kadhaa nyuma. Hapo niliongeza feni na subwoofer nikatoa kabati. Changamoto ni moja tu: Vinyozi ni vichwa vibovu haswaaa! Mbona nilifunga!
Siku ukienda kunyoa unaona wateja wanapishana tu, usipokuwepo anasema hakunyoa.
 
Mchanganuo uko vizuri sana na unaendana hasa na kitu nilichokifanya miaka kadhaa nyuma. Hapo niliongeza feni na subwoofer nikatoa kabati. Changamoto ni moja tu: Vinyozi ni vichwa vibovu haswaaa! Mbona nilifunga!
Siku ukienda kunyoa unaona wateja wanapishana tu, usipokuwepo anasema hakunyoa.
Kamera inaweza juwa msaada au hapana?
 
Back
Top Bottom