Anayesema kwamba hizi element zimefikia kiwango cha ore grade ni nani?
kiwango cha ore grade ni kipi?
Hizo maabara za kimataifa unazoziamini zina sifa gani...na je sifa ya ufisadi unaicontrol vipi?
Je acacia hajafaidika na kiwango hiki ambacho umekiita sio ore grade??kama amefaidika je kodi yetu ililipwa?kama hajalipa kwa nini?
Uwepo wa hizo elements kwa kiwango ore grade ni kiasi gani kimataifa?
Mkuu karibu ufunguke.
Accredited laboratory ni maabara ambazo zimethibitishwa kwa viwango vya kimataifa kuwa zimefikia ubora katika upimaji. Na hili si jambo geni katika fani yoyote ile. Ndiyo maana hata kwenye bidhaa za kawaida tunaongelea bidhaa zilizothibitika kukidhi au kufikia viwango vya ubora.
Kwa hiyo kuna taasisi za kitaalam za kimataifa zinazothibitisha kuwa maabara imefikia kiwango cha kimataifa. Ni maabara hizo tu ndiyo ambazo taarifa zake zinakubalika na vyombo vya kisheria na hata kwenye masoko ya fedha. Maabara hizi hazipo kwaajili ya kupima mchanga bali ni kwaajili ya kupima viwango vya elements kwa lengo lolote lile ambalo mwenye samples anataka.
Kuuliza ni nani anayeamua kuwa element fulani imefikia ore grade ni sawa na kuuliza ni nani anayeamua kuwa mtu akiwa na damu ya asilimia fulani basi huyu ni mzima na hahitaji kuongezewa damu.
Mining ni industry ambayo ina wataalam, ina tafiti na ina uzoefu. Hakuna mtu anayeamua kuwa element ikiwa chini ya kiasi fulani haijafikia ore grade bali ni utaalam ndiyo unaoamua. Unapofanya utafiti wa madini, kuna mambo kadhaa ambayo unataka kuyajua. 1) Presence of mineralization 2) Grade of the mineralization 3) Continuity 4) Style and geometry of mineralization 5) Quantity 5) Recovery 6) Metallurgy.
Baada ya hayo yote kuyajua, na kama yote yapo kwa namna nzuri, unaenda kwenye economics ambako ni pamoja na bei ya soko ya madini husika, kodi zitakazotozwa, aina ya uchimbaji na gharama zake, gharama za consumables, etc.
Hizi sababu zote kwa pamoja ndiyo zitakazokueleza kama madini uliyoyapata yachimbwe au yasichimbwe, au element fulani ambayo ipo kwenye ore yako iwe ni miongoni mwa target byproducts au iwe sehemu ya waste.
Ukija kwenye suala la PGEs zilizoonekana kwenye concentrate, Acacia walipata nini? Mimi ninavyofahamu ni kuwa walipata 0 kwa sababu haikuwa sehemu ya recovered minerals, yalikuwa sehemu ya waste. Ile waste yote inayotupwa ni minerals ambazo hazina commercial value.
Kamati ingeweza kufanya uchunguzi kama hizo elements zilikuwa sehemu ya waste au sehemu ya recoverable minerals kuliko kufikiria tu kuwa elements zote zilikuwa recovered. Mbona mchanga na mawe tunayojengea huwa hatutoi chuma, calcium au magnesium ambazo kwa uhakika zipo lakini hazijafikia kiasi cha kuwa commercially mineable.