The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,773
- 3,773
Moderator, tafadhali kwa heshima na taadhima, naomba Uzi huu ujitegemee, usiunganishwe. Nataka rafiki yangu Mch. Peter Msigwa au washauri wake wa karibu wauone kirahisi pengine naweza kumsaidia. Ni rafiki na ndugu yangu, akinisoma tu ananielewa kwa code zetu...
=====================================
Ndugu yangu na rafiki yangu Mch. Peter Msigwa;
Bwana Yesu Kristo apewe sifa mchungaji wangu...!
Hapa ulifanyaga vizuri sana kuomba radhi ulipogundua kuwa umerusha tuhuma za uongo dhidi ya Abdulhaman Kinana mwaka 2020. Hata kwa hili, unayo fursa ya kurekebisha mambo kabla hayajakuharibikia...
=====================================
Mimi hata hivyo najiuliza, ni kwanini umekubali shetani akuingize kwenye mtego rahisi lakini hatari kiasi hiki. Kwanini unajipeleka kwenye mauti ya kama afavyo mpumbavu mfano wa Abneri wa kwenye Biblia....?
Mch. Peter Msigwa, usife kipumbavu kama kamanda wa Jeshi la Mfalme Saudi, Capt. Abneri alivyokufa na Daud kumshangaa kufa vile. Mikono, akili na ufahamu wako havijafungwa. Unaweza kujiponya sasa kwa maamuzi ya hekima maana hii ndiyo silaha yako kwa sasa. Hekima na kuomba radhi, basi....
Fahamu kuwa, kuhama chama cha siasa na kujiunga na kingine wala siyo tatizo hapa......
Tatizo ni kukosa kwako kuenenda kwa hekima baada ya hapo. Na sasa ukikaa vibaya tu na ukishupaza shingo yako tu kwa sababu ya fahari ya dunia hii; pesa, umaarufu nk, nakuhakikishia jambo moja kuwa, unakwenda kuangamia kiroho na kimwili moja kwa moja muda si mrefu ...!
Mchungaji wangu hebu soma maandiko haya ktk Biblia yako👇;
Wagalatia 6:7-8 SUV
"......Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele..."
Mchungaji wangu, usidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Unachokipanda, ndicho unachovuna maana yeye Mungu keshasema hivyo.....
Nimeona "demand notice" uliyotumiwa na wanasheria wa uliyeamua kupambana naye. Ni ngumu kwako. Imeandaliwa kitaalamu kweli ikibeba kila shutuma na tuhuma zako.....
Nafsi na roho yangu mimi inaniambia, ulivuka mstari wa siasa zako na kuanza kumshambulia mtu. Na ni dhahiri kabisa kuwa, huna ushahidi wa tuhuma zako hizi......
Bahati mbaya kuwa, wewe unadhani ulikuwa unafanya siasa. Lakini siasa yako hukuiwekea mpaka kutenganisha kati ya freeman Mbowe - CHADEMA kama taasisi na Freeman Mbowe kama mtu binafsi, mwana familia na mfanyabiashara.....
Ukubali kuwa ulitoka kwenye kuishambulia taasisi na badala yake ukaanza kum - defame mtu binafsi. Kuuvuka mpaka huo ni lazima uingie kwenye mgogoro wa kisheria iwapo mtu huyo ataamua kukushughulikia. Na hivi ndivyo ilivyo Sasa......
Ushauri wangu ni huu. Ishinde AIBU na FEDHEHA kama mchungaji wako mkuu Yesu Kristo alivyoishinda aibu na fedheha ya msalaba. Soma Biblia yako 👇 👇 tena;
Ukifanikiwa hili, omba tu radhi yaishe na endelea na siasa zako huko CCM lakini ukiwa na umakini zaidi safari hii......
Tumia hekima yako ya kichungaji kufanya siasa zako. Jifunze kwa wenzio kina Tundu Lissu. Wanajua kucheza mchezo ktk mpaka wa sheria za mchezo ndio maana watesi wake wakimpeleka kwenye sheria, huwashinda kirahisi au wenyewe huzitelekeza kesi.......
Watu aina ya Tundu Lissu wanajua kudhibiti midomo yao kuwaingiza ktk migogoro ya kisheria. Wewe sijui umepagawa na nini maana aada ya kuhama CHADEMA na kwenda huko umekuwa kama kichaa fulani asiye na udhibiti hata kama atafungwa kamba za mkatale kwani miropoko yako huishangaza dunia nzima......!
Mungu akubariki, akurehemu na akupe neema ya kukufungua ufahamu wako urudi katika hali yako ya kawaida.
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Freeman Mbowe amtaka Mchungaji Peter Msigwa kumuomba radhi kwenye Magazeti na kulipa fidia ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumkashifu na kumchafua jina
=====================================
Ndugu yangu na rafiki yangu Mch. Peter Msigwa;
Bwana Yesu Kristo apewe sifa mchungaji wangu...!
Hapa ulifanyaga vizuri sana kuomba radhi ulipogundua kuwa umerusha tuhuma za uongo dhidi ya Abdulhaman Kinana mwaka 2020. Hata kwa hili, unayo fursa ya kurekebisha mambo kabla hayajakuharibikia...
=====================================
Mimi hata hivyo najiuliza, ni kwanini umekubali shetani akuingize kwenye mtego rahisi lakini hatari kiasi hiki. Kwanini unajipeleka kwenye mauti ya kama afavyo mpumbavu mfano wa Abneri wa kwenye Biblia....?
2 Samwel 3:32-34 SUV
".....Wakamzika Abneri katika Hebroni; naye mfalme akapaza sauti yake, akalia kaburini kwa Abneri, nao watu wote wakalia. Ndipo mfalme akamwomboleza Abneri, akasema, Ilimpasaje Abneri kufa afavyo mpumbavu? Mikono yako haikufungwa, Wala miguu yako haikutiwa pingu; Aangukavyo mtu mbele ya wana wa uovu, ndivyo ulivyoanguka. Na watu wote wakaongeza kumlilia....."Mch. Peter Msigwa, usife kipumbavu kama kamanda wa Jeshi la Mfalme Saudi, Capt. Abneri alivyokufa na Daud kumshangaa kufa vile. Mikono, akili na ufahamu wako havijafungwa. Unaweza kujiponya sasa kwa maamuzi ya hekima maana hii ndiyo silaha yako kwa sasa. Hekima na kuomba radhi, basi....
Fahamu kuwa, kuhama chama cha siasa na kujiunga na kingine wala siyo tatizo hapa......
Tatizo ni kukosa kwako kuenenda kwa hekima baada ya hapo. Na sasa ukikaa vibaya tu na ukishupaza shingo yako tu kwa sababu ya fahari ya dunia hii; pesa, umaarufu nk, nakuhakikishia jambo moja kuwa, unakwenda kuangamia kiroho na kimwili moja kwa moja muda si mrefu ...!
Mchungaji wangu hebu soma maandiko haya ktk Biblia yako👇;
Wagalatia 6:7-8 SUV
"......Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele..."
Mchungaji wangu, usidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Unachokipanda, ndicho unachovuna maana yeye Mungu keshasema hivyo.....
Nimeona "demand notice" uliyotumiwa na wanasheria wa uliyeamua kupambana naye. Ni ngumu kwako. Imeandaliwa kitaalamu kweli ikibeba kila shutuma na tuhuma zako.....
Nafsi na roho yangu mimi inaniambia, ulivuka mstari wa siasa zako na kuanza kumshambulia mtu. Na ni dhahiri kabisa kuwa, huna ushahidi wa tuhuma zako hizi......
Bahati mbaya kuwa, wewe unadhani ulikuwa unafanya siasa. Lakini siasa yako hukuiwekea mpaka kutenganisha kati ya freeman Mbowe - CHADEMA kama taasisi na Freeman Mbowe kama mtu binafsi, mwana familia na mfanyabiashara.....
Ukubali kuwa ulitoka kwenye kuishambulia taasisi na badala yake ukaanza kum - defame mtu binafsi. Kuuvuka mpaka huo ni lazima uingie kwenye mgogoro wa kisheria iwapo mtu huyo ataamua kukushughulikia. Na hivi ndivyo ilivyo Sasa......
Ushauri wangu ni huu. Ishinde AIBU na FEDHEHA kama mchungaji wako mkuu Yesu Kristo alivyoishinda aibu na fedheha ya msalaba. Soma Biblia yako 👇 👇 tena;
Waebrani 12:1-3 SUV
"........Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu...."Ukifanikiwa hili, omba tu radhi yaishe na endelea na siasa zako huko CCM lakini ukiwa na umakini zaidi safari hii......