Mch. Mbarikiwa ahoji iwapo kiongozi wa dini kukemea uovu wa viongozi wa kisiasa ndiyo kuchanganya dini na siasa? Amtaka Kikwete kufafanua hoja yake

Uzima Tele

JF-Expert Member
Jan 20, 2023
1,270
2,820
Ukombozi wa pili wa taifa la Tanganyika utatokea Mbeya, Singida na Kilimanjaro bila shaka..

Huyu mchungaji anaitwa Mbarikiwa Mwakipesile. Anatoka Mbeya. Hajulikani sana ktk harakati za kupigania HAKI kama walivyo kina Tundu Lissu au Mdude Nyangali au Boniface Mwambukusi au Dr Slaa au Freeman Mbowe nk nk.

Lakini huyu mtu ni kamanda kwelikweli. Ni jasusi la Mungu aliye hai, Mungu wa mbinguni...

Wakati wengine wanatumia mahakama, mikutano ya kisiasa (people's power) kama silaha za kupambana na dhuluma na kupigania haki...

Lakini Mch Mbarikiwa Mwakipesile anatumia silaha kali na hatari zaidi kuliko zote unazozijua wewe kupambana na dhuluma toka kwa mamlaka za serikali za kidunia. Silaha hizo ni MAOMBI na NENO LA MUNGU..

Hapa anapangua kombora lililorushwa na Jakaya Kikwete la kuchanganya dini na siasa. Na baada ya kupangua anaachilia upanga wa roho kupiga na kuvunja vunja...

Bila shaka Kikwete hakueleweka. Hata mimi sikumwelewa aisee..

Pia, soma
 
Mmeambiwa dawa ni kuwakalia kimya TU.

Tutapiga kelele lakini mamlaka haiwajibu yenyewe itatenda TU.

Huu mkataba ushapitishwa muda utasema.

Na tumeambiwa hakuna mwenye mabavu.
 
Huyu mgonjwa wa akili ameshamaliza kiki yake aliyojitengenezea ili apate umaarufu wa mgongo wa Mkurugenzi wa Usalama?
Yeye na wewe mko ktk ulimwengu tofauti. Huwezi kuelewa haya. Nuru na giza haviwezi kupatana. Wewe ni sehemu ya giza (ukosefu wa uelewa na ufahamu). Pole sana..

Unaweza kuwa wewe ndiwe hasa mgonjwa wa akili huku ukijidhania kuwa una hekima na nguvu kumbe ni kopo tupu kichwani..

Watu kama wewe walikuwepo hata kule Korintho ya kale.

Lakini Mtume Paulo katika waraka wake wa kwanza kwa Wakorintho, anakupa hekima na maarifa ili upanue ufahamu wako ili uepuke hukumu

"....bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;..."

1 Kor 1:27‭-‬28 SUV

Wewe unamwona Mbarikiwa kama mnyonge au dhaifu na kichaa, it's ok....

Lakini Mungu hutumia wanyonge, dhaifu na waonekanao kwa macho ya kibinadamu kama vichaa ili awaaibishe wenye hekima ya kibinadamu, wenye nguvu za kibinadamu na pia naaam, avibatilishe vilivyoko..

Wakati wa kuaibika wajionao wana hekima na nguvu, ni huu umekwisha kuwadia...

Wakati wa Kila kitu kilichopo kubadilishwa, ni huu umekwishakuwadia..

Hili ndilo NENO LA BWANA...
 
Mmeambiwa dawa ni kuwakalia kimya TU.

Tutapiga kelele lakini mamlaka haiwajibu yenyewe itatenda TU.

Huu mkataba ushapitishwa muda utasema.

Na tumeambiwa hakuna mwenye mabavu.
Mama abdul mswahili haswaaaaaa mie nimeona taarabu Tu Hana jipya japo moyo unamdunda
 
Back
Top Bottom