MC Pilipili anatrend baada ya kuachana na mkewe (kataa ndoa)

captain 6

Senior Member
May 7, 2024
127
106
ninayoandika hapa simsingizii mtu bali natoa habari zangu kwenye vyanzo vya uhakika. sasa hivi mc pilipili ana trend baada ya kutangaza kuachana na mwanamke wake na kwenda mbali zaidi kusema ana tamaa huyo mwanamke.

kwa wasiomjua mc pilipili hakukurupuka hadi kufikia hatua ya kuwa msanii maarufu na mkubwa jamaa alipambana na akajipata mwishowe akaamua kuoa huyo mwanamke wake.

mwanamke mzuri na mrembo kweli kweli kila mwanaume rijali lazima angetamani kuwa naye. yes mc pilipili akaamua kumuoa na kufanya sherehe yenye gharama kubwa sana na kufungua hadi kanisa pamoja .

kwenye akili za mc pilipili aliamini huyo ni mwanamke wake wa maisha mpka ikafikia hatua akatangaza kutamani kutoa tena mahali kwa mara ya pili yote kutokana na kuonesha kiasi gani anampenda huyo mwanamke.

mc pilipili katumia pesa nyingi sana kwenye matanuzi na huyo mke wake lakini hadi sasa wameachana mc pilipili kafunga hadi kanisa hapo unapata picha kiasi gani mc pilipili kayumba kiuchumi.

hapo sijamgusia stamina na mke wake hadi kuamua kumtolea nyimbo, bado sijamgusia mke wa masanja na katibu wake wa kanisa ambaye hadi sasa katibu hayupo tena kanisani (tetesi).

wapo matajiri wakubwa kma elon musk na bill gate walikutana na mambo hya kutoka kwa wanawake zao. bado sijamzungumzia kanye west na ugumu wake alikiri kumpa kila kitu kim lakini mwisho wa siku kim aliomba talaka.

ukisoma hapo juu utaelewa kuwa haya mambo yapo na yanatokea na sio kama yanahusiana moja kwa moja na mahusiano yangu binafsi hapana bali ni mahusiano yote kwa ujumla.

mwanamke mwenyewe hajui anataka nini muda mwengine mwanamke namfananisha kma mtoto ambaye anaomba umnunulie mdori unamnunulia kesho akienda kwa mtoto mwenzie akiona kuna mdori ambao hana yeye lazima atakulazimisha umnunulie huyo mdori.

kwa kifupi hawajui wnachokitaka wanaendeshwa na hisia zao zaidi za wakati huo ndo maan mke wa mabeste akuona shida kumuacha mabeste licha ya mabeste kumhangaikia akiwa mgonjwa.

mwanamke hajali umekuwa naye kwenye mahusiano kwa muda gani mna watoto wangapi anachojali yeye ni hisia zake kwa wakati huo. kw kifupi wanawake wengi ni wabinafsi ndo maana ukikuta mwanamke anampa pesa mwanaume jua ni mtego tu muda wowote atakukumbusha kuhusu hiyo pesa.

mwisho, mwanaume ana mengi ya kupoteza kwenye mahusiano na hata ndoa kuliko mwanamke. usiniulize kwanini diamond licha ya kutembea na wanawake kibao warembo kwanini haoi, usiniulize kwanini CR 7 haoi licha ya utajiri walionao, wote wanajua kuwa kwenye ndoa wana mengi ya kupoteza kuliko wanawake zao na usishangae kwanini wako karibu sana na mama zao.

Follow Daniel Lokamacheki
1736764448816.jpg
 
Ulikuwa na hoja… tatizo uwasilishaji!

Tatizo mi ninaloliona hapa ni moja, kwa case ya MC Pilipili, Ninamlaumu mwanamke, Ni kama kuna muda wanawake wanaolewa ili waondoe hiyo kasumba “ya kutokuolewa” baada ya hapo waendelee na maisha yao. Kwasababu WTF niolewe miaka mitatu tu? Ningeweza kufanya maamuzi ya kutokuolewa na nisipate madhara yoyote. Sorry not sorry binafsi ningeambiwa niolewe na pilipili ningekimbia nivunjike miguu. Ila Mena sababu ulimkubali mwenzio ulipaswa uishi nae, sababu watu wote tunajua alikuwa anakupenda, ulichofanya umemchezea mwenzio.

Msingi wa hoja yangu ni kwanini ndoa idumu less than 5 years? Maana yake kuna underlined issues ila mkaamua kuziignore, kila mmoja alikurupuka kwa nafasi yake ili mradi aolewe/aoe.

Binafsi siwalaumu watu wakiachana baada ya 10+ years, probably wamejaribu imeshindikana, less than this is highly questionable. (Merely opinions)
 
Ulikuwa na hoja… tatizo uwasilishaji!

Tatizo mi ninaloliona hapa ni moja, kwa case ya MC Pilipili, Ninamlaumu mwanamke, Ni kama kuna muda wanawake wanaolewa ili waondoe hiyo kasumba “ya kutokuolewa” baada ya hapo waendelee na maisha yao. Kwasababu WTF niolewe miaka mitatu tu? Ningeweza kufanya maamuzi ya kutokuolewa na nisipate madhara yoyote. Sorry not sorry binafsi ningeambiwa niolewe na pilipili ningekimbia nivunjike miguu. Ila Mena sababu ulimkubali mwenzio ulipaswa uishi nae, sababu watu wote tunajua alikuwa anakupenda, ulichofanya umemchezea mwenzio.

Msingi wa hoja yangu ni kwanini ndoa idumu less than 5 years? Maana yake kuna underlined issues ambazo mliziona ila mkaamua kuziignore, kila mmoja alikurupuka kwa nafasi yake ili mradi aolewe/aoe.

Binafsi siwalaumu watu wakiachana baada ya 10+ years, probably wamejaribu imeshindikana, less than this is questionable. (Merely opinions)
Kitu kipya nimepata hapa,,kumbe unaweza olewa kisha ukaachana na kuendelea na maisha yako,,ila tu isomeke kwa watu ulishawahi olewa🙌🏾🙌🏾
 
Back
Top Bottom