Mbunge wangu Kubenea achana na siasa za (antagonize) za kina Mnyika, utakuja kimbia Ubungo

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Mbunge wangu Saidi Kubenea, kwanza nakupongeza sisi wote tunaooishi jimbo la Ubungo mbunge wetu ni wewe kubenea na Dk. John Pombe Magufuli ndiye rais wetu.

Kubenea mimi naishi Ubungo makoka kabla ya uchaguzi hukujulikana kabisa huku kwetu Makoka, wengi walikuwa wanamjua Mnyika kama mbunge wetu ambaye anasemwa vibaya kwa kuwa alitutelekeza wana Ubungo na mwisho wa siku akakimbilia kibamba baada ya kushindwa kuyatekeleza aliyotuahidi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Mnyika alishindwa kabisa kuwatembelea wananchi wake na kuwasikiliza shida zetu hususani, kututatulia shida ya maji wana wa Ubungo, kuanzia, mwembe chai, kagera, Agentina, Manzese mpaka Ubungo na kimara yake kwa ujumla, huku nilipo mimi Makoka tulishazoea kuuziwa maji na walanguzi wanapita na magari yao wanatuuzia ndoo shilingi 500 wakati mwingine mpaka sh. 1000.

Mbunge wangu kubenea ukiweza shughulikia hili tunajua wanaotuuzia wanatoa maji katika mabomba ya serikali ukishindwa tutamfata Makonda atusaidie kwa kuwa yule ni kijana mzalendo na asiyetaka masihara akiwa kazini tunajua atawashughulikia na tatizo litakwisha ingawa tunajua hupendi kulisikia kabisa jina la mzalendo Makonda.

Mbunge wangu Kubenea nakusihi usiwe kama mbunge aliyetukimbi Mnyika, kama katibu mwenezi wa CHADEMA alitumia muda mwingi kuuza sura katika vyombo vya habari, alifurahia kutangazwa kama mwanasiasa machachari anayeichachafya serikali wakati wananchi wake tunaumia.

Ingawa na wewe umeshaanza tabia hiyo unatumia muda mwingi kushinda makao makuu ya CHADEMA pale ufipa kinondoni, badala ya kutumia muda huo kukutana viongozi wenzako pale makao makuu ya wilaya ya Kinondoni, akiwemo mkuu wa wilaya Paulo Makonda ambaye ni mwakilishi wa rais Magufuli ili msaidiane kutatua kero na changamoto za wana Ubungo.

Mbunge wangu Kubenea tangu tukuchague tumeanza kukuona ukifuata nyayo zile zile za Mnyika za kufuata siasa za kusigana na serikali (to antagonize the establishment) kama anavyofanya Lema kuliko kuwatumikia wananchi.

Mnyika na Lema wanadhani antagonize ni ushujaa, kiuhalisia huo sio upinzani na wala hauna manufaa kwa mwananchi wa kawaida, nakuusia mbunge wangu Kubenea usiige huu upumbafu kazi yako kubwa ni kututumikia wananchi na si kusigana na dola.

Mbunge wangu Kubenea tulipomuwezesha Mnyika kuwa mbunge wa Ubungo mwaka 2010, alikuwa anatumia muda mwingi kukitumikia CHADEMA badala ya sisi wananchi wake tuliyemchagua tafadhali sana usirudie kosa hilo kwani litakukimbiza Ubungo kama alivyokimbi
 
Kubenea endelea hivyohivyo achana na huyu mamluki la kijani.

umetumwa au unatumika vibaya kinyume na mabile

Kuna point moja ya halali kabisa.
Mbowe na Ndesamburo wameweza kuongoza na kuleta maendeleo makubwa na ya wazi katika majimbo yao bila kuendesha siasa za fuji, vurugu na vitimbi.
Makamanda wengine waige mfano huo na washirikiane (wakati mwingine wakabane) na watendaji wa serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi.
 
Wapiga Kura wa UBUNGO TUNAHITAJI MAJI NA KUONDOLEWA KERO ZINAZOTUKABILI MABOMBA YA MAJI YAKO KMS. MBILI TU YAFIKE MATANKI YA CHUO KIKUU AKASHINDE HUKO SITE NA YULE MKANDARASI ALIYETOKA INDIA NA WELDERS WA KIHINDI KANA KWAMBA TANZANIA HAKUNA WACHOMEA VYUMA WAMEJAA KILA KONA TABATA NA VIWORKSHOP KIBAO MAJI YAFIKE AACHANE NA HAYO MENGINE.HIVI BUNGENI ATAMUULIZA WAZIRI WA MAJI SWALI LA NYONGEZA NI LINI WAPIGA KURA WANGU WA UBUNGO WATAPATA MAJI? AFANYE ZIARA SITE IKIWEZEKANA APIGE KAMBI HUKOHUKO
 
upeo wa kubenea mdogo sana hawezi kufanya siasa za hoja bila kufanya siasa za kikatuni huwezi kumsikia maana hawezi kujenga hoja.
 
KUBENEA siasa zinamshinda asubuhi na mapema.

Na huwa wanakuja kujutia sana hawa jamaa. Nampongeza mwenzie Lwakatale sahivi kajifunza na yuko kikazi zaidi na amekuwa mnyenyekevu sana. Kabla ya hapo akiwa mbunge na KUB miaka ile alikuwa hana tofauti na Kubenea wa leo , alijiona yeye kwake ni bifu na tafrani mda wote, akawa haambiliki na hashikiki. Kwa watu wanaojitambua mtu wa hivi hafai kwa maana kuna vitu wananchi wanaviitaji zaidi ya mabifu, kilichofata anakijua Lwakas, maana mtu mzima kutoa chozi si jambo dogo lakini hakukuwa na namna tena, ni kama yaliyomkuta Kagasheki mara hii. Hizi tabia za huyu Kubenea kama hajirekebishi na wana jimbo wakasimama naamini miaka 5 itachora mstari chini.
 

sometimes we need to be serious.kazi ya kusambaza maji si ya Mbunge."kwa jiji la DSM ni kazi ya DAWASA kama owner wa infrastructure na DAWASCO kama service provider". kazi ya Mbunge ni kutunga sera zitakazokuwa implemented na serikali kupitia agencies zake, na kuzisimamia.
 
Mwache ahangaike tu kama anatafuta danga akijakushtuka ni wakati wa uchaguzi na tutamnyoosha!!
 
Wabunge wa ukawa wafanye kaz za maendeleo kwenye majimbo yao kwa nguvu zote ili wananchi waone mabadiliko chanya,nampongeza prof Jay huwa anashinda mikumi huko anasaidiana na wakandarasi kujenga barabara za vijijini hayo ndiyo mambo wananchi wanayotaka ili mjihakikishie ushindi tena mwaka 2020.
Kuibua ufisadi ni jambo jema lakini lifanywe kwa kubalansi;huku wananchi wanaona maendeleo lakini huku pia ufisadi unaibukiwa sio kukomaa na ufisadi tu lakini wananchi bado wanakuwa na shinda chungu mbovu
 

Kubenea ni sawa na sikio la kufa halisikii dawa
 
Tatizo ya team mitandao ya manguruwe ya ccm ndiyo hiyo Kubenea kawabana ukutani mutaanzisha thread na thread kwa kila sampuli ya IDs mulizonazo na hiyo ndio safiii kwa mbunge wa ubungo anapandishwa chati na team mtandao ccm
 
na serikali inayokusanya kodi ifanyeje ikalale chato
 
na serikali inayokusanya kodi ifanyeje ikalale chato

Simaanishi kuwa serkali ikalale au la,kaz kubwa ya mbunge ni kuishinikiza serkali ipeleke maendeleo kwenye jimbo lake.wabunge wa ukawa wanatakiwa muda wote wakomae kuishinikiza serkali itatue changamoto zilizopo kwenye majimbo yao.Watu wanataka maendeleo sivinginevyo
 

Unaposema Mnyika amekimbia amekimbilia wapi?

Technically, Mnyika kagombea Ubongo 2015. Wananchi waliompa kura 2010 ndio hao hao wamempa kura 2015. Au ingeitwa Ubungo A na Ubungo B badala ya Kibamba ndio ungeelewa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…