Salamu Mheshimiwa John Mnyika John. Please angalia changamoto zetu hapo chini na uje huku mashinani tutatue changamoto hizi pamoja.
Barabara
Sisi wakazi wa maeneo tajwa hapo juu tunachangamoto kubwa sana ya barabara ya kutoka Mbezi mwisho kwenda either Makabe, Msakuzi na Msumi. Sikumbuki barabara hizi zilitwengenezwa lini? Kifusi na kokoto kilichowekwa miaka takribani mitano iloyopita kimeondoka na yamebaki mawe ambayo yahaharibu magari yetu. Hii imepelekea dala dala kupungua kwa kiasi kukubwa na nauli ni shilingi 1000. Please do something wakati wa kampeni ulituaidi lakini yawezekana bado unalifanyia kazi. Tupatie mrejesho tafadhali.
Maji
Bado maji ni kitendawilli kwenye maeneo tajwa. Huku bado utaratibu wa malori umekuwa ndo suluhisho. Kwa kufuatia adha hii watoto wa watu masikini/ kipato cha chini wanaogo mara moja kwa wiki. Uniform ni chafu na wengi wanasumbuliwa na magonjwa ya ngozi. Kama tungekuwa maeneo ya mabondeni basi kungekuwa na mlipuko mkubwa wa magonjwa ya kuambukiza. Tunashukuru Mola kwamba huku kipindu pindu sio sana.
Upimaji wa maeneo/ Urasimishaji wa maeneo
Maeneo mengi takribani asilimia 99.99 hayajapimwa. Gharama ya kupima eneo ni shilingi milioni tano. Kwa mtanzania masikini ni ngumu kutekeleza. Hivyo basi imekuwa ni ndoto kwa mtu masikini kuwa na umiliki halali wa eneo usika. Sito shangaa tukaja kuambiwa kwamba sote ni wavamizi pindi wakitokea wawekwezaji wenye hela za kutosha.
Agalizo
Ninapoandika ujumbe huu ninajua wajibu wangu kama raia mwena na siamini kwamba hatuna wajibu wa kufanya katika kutatua changamoto hizi zinazotukabili. Wengine watanishambulia kwamba sio kazi ya mbunge kutatua changamoto hizi. La hasha ninaamini kwamba kupitia wewe unaweza ukatuunganisha watu karibu na watu wakajitokeza kwa wingi katika kushiriki hizi shughuli za maendeleo.
Jaribu kuangalia marehemu Deo Filikunjombe alifanya nini kwa wananchi wa Ludewa. Pia jifunze kwa zito kabwe kwani ni mbunge ambaye kila mara anawaandikia watu wake akiwajulisha amefanya nini na nini matarajio yake kwenye siku za usoni.
John Mnyika John Mh. tunafahamu kwamba wewe ni mchapakazi achana na kuongoza chama pekee njoo huku mashinani tujenge kibamba yetu.
Naomba kuwasilisha.