Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,695
- 1,242
MBUNGE WAMBURA CHEGE: "SITARUDI NYUMA, NIMECHAGULIWA NA WANANCHI LAZIMA KUWATUMIKIA"
"Tumezaliwa tunazungumzia changamoto za Madaraja, Maji na maeneo mengine. Nimeamua kujikita kwenye shughuli za Maendeleo lakini kuna watu wanapita kutafuta namna ya kutugawa. Naomba tushirikiane tushikamane tuweze kufikisha mbali Maendeleo ya watu wa Rorya" - Mhe. Jafari Wambura Chege Mbunge wa Jimbo la Rorya.
"Watu wa Kigunga na Kilogo ndiyo wanufaika wa kwanza wa Madaraja Mawili ya mto Maya na mto Mori. Tumehaingaka sana kuyapata, tukayaomba mpaka yakajengwa. Niwaombe tuendelee kukisemea Chama Cha Mapinduzi, endeleeni kumsemea na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan"
"Madaraja ya mto Maya na mto Mori mmeyaomba hata kabla mimi sijazaliwa. Tumekuja kuyajenga kwa miaka mitatu ya Dkt. Samia Suluhu Hassan. Endeleeni kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan ili miradi mliyoisema iweze kukamilika"
"Kigunga mmesema tulivyosaidiana kujenga Sekondari na nikawasaidia kupata Mifuko ya Saruji 100, nakumbuka niliwapa na Madawati kuhakikisha watoto wanakaa pamoja Diwani ambaye anajituma sana kwenye shughuli zote. Nampongeza Diwani kwa kazi nzuri anayoifanya"
"Vijana wamesema wana kibanda na wameomba wapate mabati Sita. Kesho jioni mje mchukue mabati kwaajili ya kupaua kibanda. Na mimi nawapa mabati yote Sita ili mkae sehemu yenye kimvuli mfanye kazi"
"Watu wa Masala nitawashika mkono nitawapa mifuko ya Saruji 50 kwaajili ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari na nitawapa Shilingi 500,000 muanze kujenga yale matofali yaliyopo. Nawapongeza watu wa Masala na Randa kwa kuanza Ujenzi wa Shule za Sekondari" - Mhe. Jafari Wambura Chege, Mbunge wa Jimbo la Rorya
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-07-25 at 06.03.03.jpeg70.6 KB · Views: 5
-
WhatsApp Image 2024-07-25 at 06.03.06.jpeg67.9 KB · Views: 5
-
WhatsApp Image 2024-07-25 at 06.03.06(1).jpeg90.4 KB · Views: 5
-
WhatsApp Image 2024-07-25 at 06.03.07.jpeg62.7 KB · Views: 5
-
WhatsApp Image 2024-07-25 at 06.03.08.jpeg80.6 KB · Views: 6