Mbunge: Wafugaji tusipowadhibiti watafuga ng'ombe hadi ikulu

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,969
Mbunge wa Nkasi Kaskazini Ally Kessy alipuka bungeni, asema wafugaji wakiachwa watachunga ng’ombe hadi Ikulu.

Mbunge huyu amedai kuwa wafugaji wanachangia kuharibu sana mazingira, ni lazima wadhibitiwe wafuate sheria na watu waache huruma na kuwatetea kila mara wanapochukuliwa hatua.

Amesema ufugaji wa Tanzania hauna tija na ufanisi na ng'ombe wake wamekonda na akaulinganisha na ufugaji wa nchi ya Denmark ambapo kuna ng'ombe wachache na wana ufanisi mkubwa.

 
Ni mjinga tu, hajitambui, na akitoka nje ya bunge anaagiza bia na supu ya mbuzi au ng'ombe.
Hatuna mfumo unaotuwezesha kufuga kama Denmark.
Hatuna :
Elimu ya kufuga hiyo aina ya ng'ombe au mbuzi.
access ya kupata aina hiyo ya mbegu.
MASOKO yanayoridhia na kuhimili ukubwa wa uzalishaji wa ng'ombe hawa.
Mazingira rafiki ya kufugia mifugo hii.
MADAWA, maabara na madaktari wenye sifa ya kuhudumia aina hiyo ya mifugo.

Huyu jamaa na Agness uelewa ni mmoja, sema yeye anaweza kuwa na kipato zaidi.
 
Aende Denmark, anafanya nin hapa kwetu, huyu mzee anakuwaga na shida kwel sijui kwa nin, mifugo muhimu pia. Wafugaji wangetambuliwa, mifugo ikawa ina maeneo maalum, ikawa inatunzwa na kutibiwa, wafugaji wangekuwa na fedha za kufanya biashara zingine pia, sababu wangekuwa na access na mitaji. Wanyama ni asset, Ng'ombe mmoja asiye na matatizo hapungui 500,000 kama mtu anao 1000, ana value ya mil 500 kama mambo yamewekwa vizuri huwez kukosa mkopo benki hata mil 200.
Mambo ya binadamu ni kukaa chin na kujua nin kifanyike sio kupiga mdomo tu.
 
hajui kuwa hao hao ng'ombe wanatusomeshea watoto wetu, wanatuoza wake wazuri, wanatufanya tuishi bila wasiwasi maana kwetu hiyo ni social security nzuri achana na hizi za kipuuzi za NSSF etc.

bila ng'ombe kwetu ni sawa na kuishi mfu, kula chakula bila maziwa kwetu haujala, tuna akili nyingi darasani kwa sababu tunakula vizuri kwa sababu ya ng'ombe.

aache upumbavu.
 
Sio kwamba namuunga mkono kuilinganisha elimu yetu na ya Denmark lakini nadhani ni wakati umefika sasa, Wafugaji wetu wakapewa semina elekezi wajue kuwa; Watu wameongezeka sana Tanganyika, hivyo kuna shida ya ardhi ya kulishia wanyama kiholela' Wakati umefika, serekali irudishe ardhi kwa watu, watu wapewe ardhi ya kiasi na iwe imepimwa. Mtu aitunze mipaka yake mwenyewe aweze kupewa hati miliki aitumie kama dhamana bank.
Nadhani, hatua hizi chache tu, zitawafanya wafugaji wapunguze mifugo waweze kufuga kiasi cha kutosheleza ardhi aliyopimiwa.

Natamani wafugaji waelewe kuwa, kwa sababu macho yanawaonesha mbuga tupu ndo maana wanaona kuwa wana uwezo kufuga ming'ombe isio na idadi kwani majani yapo. Yeye anaona ng'ombe kushiba ndio furaha hata kama amekula mahindi ya mkulima. Haya ni mawazo potofu. Kila mtu apewe ardhi yake mwenyewe ailime, aitunze.

Nimeenda Moshi - Kilimanjaro (Machame) nikakuta watu wanafuga ng'ombe 5 tu anauza maziwa kila siku zaidi ya lita 100. Nikaenda Manyara - Simanjiro nikakuta mmasai ana ng'ombe zaidi ya 300 lakini anashida ya maziwa ya kunywa nyumbani kwake. Huu sio mfano mzuri. Kama ni nyama nadhani Kilimanjaro wanakula nyama laini sana, Manyara nyama ngumu mno. Hii sasa ni shida. Wafugaji badilikeni
 
Nadhani watu wasio wadau wa uhifadhi hawawezi kuelewa! Ufugaji nchi hii ni holela sana, wengi wao hawajali lolote usipokua mifugo tu basi! Mapori yaliyohifadhiwa yanapaswa kulindwa yasiharibiwe, wao wanachungia mifugo yao, Misitu inateketea, vyanzo vya maji vinakauka, na sasa Mapori ya akiba nayo yanayoyoma, vurugu kila upande wa nchi ni wao tu. Lazima tufike mahali ambapo watu wote tutii sheria.
 
Hoja ya Mhe Kessy ni muhimu sana na wakati umefika sasa tuwe wakweli kuhusu ufagaji katika nchi hii. Bado watu wanahama hama, wafugaji wana hali mbaya sana na wamegeuka kuwa watumbwa wa wanyama wao. Mtu ana ngombe 300 lakini hana maziwa, nyumba ni mbavu za mbwa, watoto shule tabu sasa unajiuliza hao mifugo wanamsaidiaje?
 
Huyu kessy hili Nina walikosea kumpa wazazi wake.hanaga akili timamu mkichwa vizuri sana, in km yule Agness marwa tu.
 
Ana hasira na wasukuma bure tu maana ndo wamejazana huko Nkasi na maeneo mengi ya Mkoa wa Katavi, ila hatafanikiwa, watoe elimu kwanza kwa wafugaji pamoja na mazingira wezeshi ya kumusaidia mfugaji.
 
Huyu mbuge ana hoja ya msingi na malalamiko ya wafugaji nayo yana uzito wake. Kitu cha muhimu ni serikali ihakikishe wafugaji wana maeneo ya kutosha na wawaelimishe do's and dont's. Baada ya hapo wakikiuka wasimamie sheria on point.
 
huyu mzee ana hoja ya muhimu sana ila itakwenda hivi hivi.
tunahitaji kubadili namna ya kufuga ili tuwe na manufaa. haiwezekani watu wanalisha tu mahindi ya wakulima aaafu tunaita wafugaji.
wakati huo huo wanataka kula ugali.
tusipojiangalia mkoa kama rukwa ambao ulikuwa na uzalishaji mkubwa wa mahindi utakuwa na njaa
 
You can't compare Tanzania na Denmark mr mp,ranch zetu zimeliwa tens na Hao Hao viongozi wa serikali,nakumbuka late 80s Kuleng'wa kijijini kwetu utegi, mean kanda maalum,tulikuwa na ranch Kubwa sana,ngombe walikuwa waki changwa na farasi,I mean Kama Texas vile,ukifika pale utegi kulikuwa na makazi ya wafanyakai wa sekta mbali mbali.kuanzia madereva,cow boys ,nk.
Leo hii wako wapi?ukipita barabara ya kutoka mwanza Shinyanga,unaweza Kulia kuna ranch ya (bubiki) iko empty wamelamba ngombe wote
 
Anachosema ni kweli tunatakiwa kuwa na ufugaji wenye tija na sio huu unaohusisha uharibifu wa mazingira. Tuangalie vizazi vijavyo hii ni kwa mkulima pia tukomeshe kilimo cha kuhamahama kwani nacho kinaharibu mazingira
 
Iwe ni marufuku kutoa mifugo kutoka wilaya moja kwenda nyingine kutafuta malisho. Ufugaji wa kuhamahama ukomeshwe Tanzania.
 
Ufugaji ni tatizo ambalo linakuwa siku hadi siku-bahati mbaya wengi wetu hatunauelewa mzuri kuhusu mbinu za ufugaji zinavyotawaliwa na ecologia. Na wengine wanawageuza wafugaji kuwa mitaji yao, matokeo yake tumekuwa na sera mbovu kuhusu ufugaji na haya tuyaonayo leo (aliyosema JK, anayosema Kessy, mapigano kati ya wakulima na wafugaji etc) yametokana na sera za miaka mingi nyuma ambazo zimechangia kupunguza maeneo malisho ya mifugo, kuwa na uhamaji wa masafa marefu usiokuwa na udhibiti. Tatizo hili lisipotatuliwa kisera na kwa umakini litaisumbua sana hii nchi. Itabidi tujue sehemu gani inafaa ufugaji wa aina gani na tuwekeze ipasavyo. Kwenye sehemu za ukame hakutakuwa na ufugaji endelevu kama utazuia uhamaji (masafa mafupi ya ki-ekologia) wa misimu wa kutafuta maji, malisho na madini. Huyo ngombe wa Danmark ukimpeleka huko atakuwa dhoofu bin taabani kama hatakufa. Huko swala la ranch ni ndoto kwa uchumi wetu. Sera za mali asili hasa hifadhi za wanyama pori vs ufugaji wa uchungaji zinatakiwa ziangaliwe upya na kwa umakini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…