Mbunge wa wananchi Jimbo la Chumbuni CCM Mhe. Ussi Salum Pondeza amegawa sadaka ya futari kwa watu wenye ulemavu zaidi ya 70 wanaoishi katika jimbo lake ili kusaidia katika mahitaji ya chakula katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Pondeza kupitia taasisi ya Pondeza Foundation hukutana na kuwasaidia watu wa makundi mbalimbili kwenye kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Katika maelezo yake Pondeza amesema kwa mwaka huu anatarajia kufikia watu 3,000.