Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,618
- 1,198
"Mheshimiwa Rais kwenye bajeti ya mwaka 2023-2024 amesema, Mfanyabiashara yeyote anayedaiwa kodi kwamba hajalipa TRA ni marufuku kumfungia biashara yake. Hii itumike kwa Wavuvi, Mvuvi ambaye hajalipa Shilingi 5,000 anahangaika kuvua apate Shilingi 5,000 akulipe hatuoni sababu ya kukamata chombo chake mpaka siku atakapolipa" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Kama Mfanyabiashara ambaye hajalipa kodi asifungiwe biashara yake maana mkifunga Ofisi yake hataweza kufanya biashara, hiyo kodi mnayomdai atailipaje? Huyu Mvuvi ukichukua chombo chake ukakificha atakulipaje hiyo Shilingi 5,000" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Naomba niongee na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, akiridhia ninachomuambia basi maelekezo watapewa Maafisa Uvuvi, wakuache ufanye biashara ili wakati unafanya kazi ili ulipe hiyo kodi kuliko achuke Mtumbwi wako halafu akuambie nenda katafute fedha . Unatafuta wapi wakati kile ndiyo chombo chako kinakufanya uishi, uweze kula, uhudumie familia yako, ulipe na kodi" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Nawaambia wale Maafisa Uvuvi waache hii kitu, wakudai, wakupe madai yako uendelee kutafuta fedha ili uweze kuwalipa lakini siyo wakunyang'anye chombo waende wakakifungie halafu waendelee kukudai, hili haliko sawasawa" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya