Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,016
- 5,280
Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mhe Abubakar Asenga amesema kuwa hawezi kuchukua fomu ya Kugombea ubunge wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025 kama hatokamilisha ujenzi wa Barabara ya Kata ya Lumemo ambayo imekuwa kero Kwa wananchi wa eneo Hilo
Mhe. Asenga ameyasema hayo Februari 2,2025 Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro baada ya kumaliza zoezi la kutoa msaada wa vyombo vya kupikia Kwa vijana wa eneo Hilo ambapo vijana hao pia walimuelezea kero ya barabara hiyo ambayo ni tegemeo kubwa Kwa wanakijiji na wanafunzi
"Sitachukua fomu ya ubunge kama sitakamilisha ukatabati wa Barabara hii kwani nitaonekana wa ajabu nikishindwa kuweka sawa eneo hilo" - Mhe. Abubakar Asenga
Awali baadhi ya wananchi wa eneo hilo wameeleza kero wanayopitia kutokana na barabara hiyo ambao wamesema imekuwa shida Kwa wanafunzi kwenda shuleni na hata wakulima wanaokwenda shambani Kwaajili ya Shughuli ya Kilimo kutokana na barabara hiyo kuwa tegemeo kubwa