Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini, Abdul Aziz Abood amefanya ziara ya kikazi kwenye kata ya K/Ndege

Oct 8, 2023
37
17
Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abdul Aziz M. Abood 28/11/2023 amefanya ziara ya kikazi kwenye Kata ya U/TAIFA NA K/NDEGE.

Lengo ya ziara hii Mhe Mbunge kwanza ni kusikiliza kero za wananchi kwenye mitaa ya Kata hizo, pili ni kutatua na kutoa majibu pamoja na kuwaambia wananchi wa Kata hizo kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mhe Mbunge
ameongea na wananchi wa kata hizo kwa muda tofauti na mikutano tofauti, akiwa kwenye mkutano wa Kata ya U/TAIFA Mhe Mbunge amesikiliza kero za wananchi na kuzitatua kero hizo papo kwa papo na kero zingine amezichukua ameahidi kuzifanyia kazi.

Kata ya K/NDEGE, Mhe Mbunge akiwa kata hii amekutana na maelfu ya wananchi waliyokuja kumsikiliza Mbunge wao Kipenzi, kwenye Kata hii Mhe Mbunge amepokea kero na kuzijibu, Vilevile Mhe Mbunge ametoa HUNDI ya Tsh 1,200,000 MILIONI MOJA NA LAKI MBILI kwaajili ya kununua Tofari elfu moja 1,000 ikiwa ni kusapoti nguvu za Wananchi kwa ujenzi wa Shule ya Msingi Sabasaba (B) unaoendelea.
IMG-20231128-WA0000.jpg
 
 IUchaguzi Unakaribia Sasa, Apumzike Sasa Asimamie Basi Zake Tu Maana Amekuwa Wa Kudumu Hata Jiwe Alimwambia Wazi Wewe Viwanda Vya Serikali Unafugia Mbuzi
Unangoja Watu Wafe Ukazike Na Bus Lako
 
Ulivyotaja HUNDI nikajua katoa Bilionisasa MILIONI MOJA NA LAKI MBILI nayo inahitaji HUNDI kweli??si angetoa tu cash kupunguza foleni Bank!!!kwanza kwa mipesa aliyonayo hiyo 1,200,000 hata yule mvuta bangi Seleman Msindi anaweza kutoa
 
Back
Top Bottom