Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,072
- 5,468
Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini (CCM) Mhe. Kwagilwa Rubeni, amesema kuwa wabunge na wananchi wa ukanda wa kaskazini wanaunga mkono uamuzi wa serikali wa kununua umeme kutoka Ethiopia kupitia Kenya, kwani baadhi ya maeneo ya kanda hiyo hayana vyanzo vya kutosha vya umeme.
Akizungumza na wanahabari leo, Machi 16, 2025, jijini Dodoma, Mhe. Rubeni amesema kuwa wanaopinga mpango huo hawana uelewa wa hali halisi ya mahitaji ya nishati nchini. Amebainisha kuwa Tanzania si nchi ya kwanza kununua umeme kutoka nje, akitaja mifano ya mataifa kama Marekani, India, Afrika Kusini, na Kenya, ambayo pia hununua na kuuza umeme kwa nchi jirani kutokana na jiografia na mahitaji yao ya nishati.
Amesema kuwa mpango huu utaimarisha upatikanaji wa umeme kwa maeneo yanayokabiliwa na changamoto za nishati na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.