Mbunge Ummy afanya mkutano wa hadhara kata ya nguvumali.

iamwangdamin

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
851
1,783
#OdoUmmyJimboni #SamiaMitanoTena
----
MBUNGE UMMY AFANYA MKUTANO WA HADHARA KATA YA NGUVUMALI.

Mbunge wa Tanga Mjini Mhe Ummy Mwalimu tarehe 27/07/2024 amefanya Mkutano wa hadhara kata ya Nguvumali kwa ajili ya kueleza Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha 2020 - 2025.

Wakiongea katika Mkutano huo Mhe Ummy na Diwani wa Nguvumali Mhe Selebosi Mustafa Muhina walieleza utekelezaji wa Ilani katika ya Elimu ikiwemo Sekondari ya Nguvumali, Galanosi na Shule ya Msingi Gofujuu. Pia wameelezea uboreshaji wa huduma za afya ikiwemo Uboreshaji wa Zahanati ya Nguvumali, Vituo vya Afya na pia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bombo. Aidha wameeleza jitihada zilizofanywa kuboresha upatikanaji wa maji, Miundombinu ya barabara, Umeme na Uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi.

Mhe Ummy amesema kuwa kati ya yote hayo, wanajivunia sana kazi kubwa na nzuri ya maboresho ya Bandari ya Tanga iliyowezesha kuanzia Julai 2023 meli kubwa takribani 32 kutia nanga Bandari ya Tanga na hivyo kupelekea kuongezeka kwa ajira za vibarua kutoka watu 7,000 kwa mwezi mpaka 14,000 kwa mwezi. Mhe Ummy na Mhe Selebosi wamemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Uongozi wake mahiri na uliowezesha utekelezaji wa miradi mingi ya Maendeleo kata ya Nguvumali na Jimbo la Tanga Mjini.

Pia Mhe Ummy alitoa kiasi cha pesa shilingi milioni tatu na nusu kwa vikundi vya vijana ili kuchangia miradi yao ya kujikwamua kiuchumi.

Mkutano huo wa hadhara ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Bakari Mkoba, wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya Tanga, Waheshimiwa madiwani wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe Abdurahmani Shiloo na viongozi mbalimbali wa kata ya Nguvumali. Kabla ya Mkutano wa hadhara Mhe Ummy alifanya Kikao cha ndani cha Halmashauri Kuu ya Kata ambapo wajumbe walimpongeza Mhe Rais, Mhe mbunge na Mhe diwani Mustafa Mhina Selebosi kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa Ilani.

Imetolewa na ;-
Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Tanga Mjini.
28/7/2024.




iamwangdamin
CCM OYEEEEEE CCM MBELE KWA MBELE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…