Mbunge Tawfiq: Biashara kati ya Zanzibar na Bara ni Kama Nchi Ziko Vitani

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
54,351
64,379
Bwana Mbunge ameeleza sintofahamu iliyopo kati ya Zanzibar na Bara kwenye Biashara Kwa sababu Kuna utofauti mkubwa kiasi kwamba maingiliano ya biashara ni kama Nchi ziko Vitani wakati ziko kwenye Muungano

---
Mbunge wa Jimbo la Mpendae Unguja @toufiqsturky amesema Zanzibar kuna changamoto kubwa sana kwenye upande wa biashara, Mfanya biashara anaponunua bidhaa zake Zanzibar anachuka VAT analipa aslimia 15 anapochukua biashara hiyo nakuja bara anatakiwa tofauti ya asilimia 3 inakua asilimia 18

Amemuomba Waziri wa Fedha kuhakikisha mifumo ya wizara ya fedha inaenda na mifumo ya mamlaka ya mapato Zanzibar ZRA


My Take
Dawa ni kuwa na Muungano wa Nchi Moja.

View: https://twitter.com/earadiofm/status/1803654724836540514?t=goYwoNGKDz19yyB6FmrLxA&s=19

PIA SOMA
- Mbunge Mohamed Issa: Wanaotoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar wawe na Passport

- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?
 
Na wanaopigwa vita ni watu wa huku bara.
Ukiwa Mbara kupeleka product yeyote kuuza zanzibar ni shida hata kama mtu anauhitaji wa biashara yako haji kununua kwako.
Ila mzenj kuja bara kufanya biashara ni rahisi wamejazana gerezani wanauza spere used za magari, wamejazana mitaani huku wanauza juice za miwa bila bughuza yeyote.
Mbara kajaribu biashara zenj lazima ufilisike.
Mbara zanzibar labda ukafanye kazi kwenye hoteli za wageni kama mpishi au mlinzi ingawaje nayo wanalalamika sana kwamba wanachukuliwa kazi zao wakati wao ni wavivu sana kufanya kazi hizo.
Wazanzibari ni matatizo sana huu Muungani Nyerere alituingiza chaka
 
Bwana Mbunge ameeleza sintofahamu iliyopo kati ya Zanzibar na Bara kwenye Biashara Kwa sababu Kuna utofauti mkubwa kiasi kwamba maingiliano ya biashara ni kama Nchi ziko Vitani wakati ziko kwenye Muungano

View: https://www.instagram.com/reel/C8aHTyBqyYE/?igsh=ODhuYnd5M3hic2Ez

My Take
Dawa ni kuwa na Muungano wa Nchi Moja.

Pia soma Mbunge Mohamed Issa: Wanaotoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar wawe na Passport

Kwani Tundu Lissu si anawambia kila siku?
Zanzibar wanaifaidi watu wenye vyeo kwenye serikali ya Muungano tu na hao ndio wanakwambia Muungano utalindwa kwa gharama yoyote.
 
Chukua sukari kiroba cha kilo 50 njoo nacho bara kutoka zanzbar
Yaani ni bora uagize brazil
Yaani uta tritiwa kama mjukuu wa escoba
Sion urahis wa biashara ya zanzbar ba bongo land
Sisi wafrika tuna roho mbaya sana.

Eti Sukari Bakhressa anasafirisha kutoka Brazili umbali mrefu sana kwa meli hiyo hiyo sukari ina bei nafuu kuliko inayotoka Mtibwa na Kagera.
Trump alikuwa sahihi
 
Kuna mambo mengi sana Nyerere baba wa taifa hili alisahau tu kuyasema

Aliposema kwamba, Madini yasichimbwa hadi hapo watanganyika watakapopata akili maana hayaozi, ilibidi asemee na hili la Muungano wetu pia, Watanganyika watakapokuja kuwa na akili na watakapokuja kugundua kwamba Tanganyika yao imetumika na inatumika kwa kiasi kikubwa mno kunufaisha watu wa Visiwani ilihali wao hawautaki muungano, haki ya nani watazidai mali zao kwa nguvu zote
 
Back
Top Bottom