Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 464
- 1,132
Aidha Shigongo amesema kama wakiweza kuokoa maisha ya mtu mmoja ni faida kubwa sana kwa Taifa letu. Licha kulizungumza Bunge bado kuna visa vya watu kuliwa na mamba.
Kwa upande mwingine amesema Serikali imejenga vizimba vinne ndani ya ziwa katika sehemu ya Nyachitale, Nyakalilo, Hizindabo na kizimba cha Kanyala.
Soma Pia: TAWA yafanya msako wa mamba tishio kwa maisha ya binadamu Rufiji
Mbunge Shigongo ametoa ushauri kwa Serikali kwamba waipeleke miradi ya Maji katika maeneo hayo ili kupunguza matatizo ya watu kuliwa na mamba kila siku. Maana shughuli nyingi za nyumbani zitafanyika nyumbani na hawatoenda ziwani tena.