Mbunge Saashisha Aungana na Askofu Dkt. Shoo Katika Zoezi la Upandaji wa Miti Jimbo la Hai

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,588
1,190

MBUNGE SAASHISHA AUNGANA NA ASKOFU DR. SHOO KATIKA ZOEZI LA UPANDAJI MITI HAI

Mbunge wa jimbo la Hai Mh. Saashisha Mafuwe ameshiriki katika zoezi la upandaji wa miti katika eneo ambapo kinajengwa chuo cha Kumbukumbu ya Mtakatifu Stephano Kampasi ya Machame huku akitoa wito kwa jamii kuyatunza mazingira ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Mafuwe amesema kuwa mbali na kupongeza juhudi zinazofanywa na kanisa kupitia Baba Askofu Shoo bado jamii nzima inao wajibu wa kushiriki kikamilifu katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira ili kurejesha uoto wa awali pamoja na theluji iliyoanza kupotea katika mlima Kilimanjaro.

“Nikupongeze sana Baba Askofu Shoo kama kiongozi wa kanisa umekuwa mstari wa mbele kusaidia kuyatunza mazingira yetu pamoja na majukumu makubwa uliyo nayo ya kikanisa bado pia umeshiriki nasi katika jukumu hili la uhifadhi na utunzaji wa mazingira” Alisema Mafuwe.

Awali akizungumza katika ufunguzi wa upandaji miti katika eneo hilo mkuu wa kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dr. Shoo amesema kuwa hadi kufikia sasa zaidi ya miti elfu moja imepandwa katika eneo la kampasi hiyo huku akisema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu katika uhifadhi wa mazingira.
 

Attachments

  • IMG-20230708-WA0021.jpg
    IMG-20230708-WA0021.jpg
    91.4 KB · Views: 4
  • IMG-20230708-WA0024.jpg
    IMG-20230708-WA0024.jpg
    153.7 KB · Views: 4
  • IMG-20230708-WA0022.jpg
    IMG-20230708-WA0022.jpg
    166.1 KB · Views: 4
  • IMG-20230708-WA0025.jpg
    IMG-20230708-WA0025.jpg
    153.8 KB · Views: 4
Back
Top Bottom