Kuelekea 2025 Mbunge Norah Mzeru agawa simu janja (Smartphone) kwa UWT Wilaya ya Kilosa ili kusaidia kusajili Wanawake katika Mfumo wa Kielektroniki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,664
1,228

MHE. NORAH MZERU Agawa Simu Janja (Smartphone 📱) kwa UWT Wilaya ya Kilosa Ili Kusaidia Kusajili Wanawake Katika Mfumo wa Kielektroniki

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Waziri Mzeru tarehe 01 Mei, 2024 amegawa Simu Janja 5 (Smartphone 5) kwa uongozi wa UWT Wilaya ya Kilosa na Tarafa zake ili kusaidia Kusajili wanachama wapya wa jumuiya ya UWT katika mfumo wa Kielektroniki uitwao CCM App

Mhe. Norah Waziri Mzeru amesema kuwa amekabidhi Simu Janja ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mwenyekiti wa UWT Taifa, Ndugu Mary Pius Chatanda aliyoyatoa kwa Wabunge wa Viti Maalum kutaka kila Mbunge kuchangia manunuzi ya simu za Smartphones, hivyo ametimiza ahadi yake.

"Ndugu zangu viongozi wa UWT nawaomba sana simu hizi zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na siyo kwa matumizi yetu binafsi nawaomba mjitahidi kupata wanawake wengi katika mitaa mnayoishi, sisi wanawake ni jeshi kubwa na katika chaguzi zetu asilimia kubwa ya wapigaji kura ni wanawake. Tutakapopata idadi kubwa ya wanawake tutakuwa tumepata mtaji mkubwa" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Sisi wanawake tupendane na utakapoona mwanamke mwenzetu anafaa tumshawishi kugombea ili tupate wanawake wengi kwenye Vitongoji na Vijiji tuendelee kumtafutia kura nyingi Mheshimiwa Rais wetu katika uchaguzi mkuu 2025" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

Norah Mzeru amewaomba Wanawake kuendelea kumsemea vizuri Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuendeleza miradi mikubwa ya maendeleo nchini.

Mhe. Norah Mzeru amekabidhi simu janja hizo kwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Morogoro, Ndugu Alice Libenanga na kushuhudiwa na viongozi wengine akiwemo Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kilosa, Ndugu Jamila Miyonga.

Mwisho, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya ya UWT Mkoa wa Morogoro wamempongeza sana Mbunge Mhe. Norah Waziri Mzeru kwa moyo wa kujitolea wa kuimarisha Jumuiya ya UWT kwa kutoa simu za kusajili kielektroniki wanachama wapya wa jumuiya hiyo.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

WhatsApp Image 2024-05-02 at 08.04.36(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-05-02 at 08.04.34.jpeg
WhatsApp Image 2024-05-02 at 08.04.35.jpeg
 
Huyu mume wake ni Yule alikuwa anatembea na BLACK BAG ….agents paymaster wa TISS …. Alichezea pesa ya idara sana …..kwa mambo ambayo hayakuwa na state interest …., alikuja kupigwa risasi mchana peupe pale uwanja wa ndege ….alikuwa pia na kashfa ya kusaidia Wauza unga kuvuka uwanja wa ndege kupitia mtandao wake …..Kaacha nyumba nyingi sana ambazo siddhani Kama familia yake itaweza kuzipata zote
 
Back
Top Bottom