Mbunge Munira Mustafa Khatibu Akabidhi Matofali 2,000 Ujenzi Miradi ya UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,687
1,238

Mbunge Munira Mustafa Khatibu Akabidhi Matofali 2,000 Ujenzi Miradi ya UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar

Mbunge wa Viti Maalum Kundi la Vijana Taifa Mhe. Munira Mustafa Khatibu amekabidhi Matofali 2,000 kwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Ndugu Ismail Ali Ussi kwaajili ya ujenzi wa Maduka na nyumba ya mtumishi ya Mkoa wa Kaskazini Kinduni Zanzibar.

Mhe. Munira Mustafa Khatibu alikabidhi jumla ya Matofali 2,000 katika Mkoa wa Kaskazini Unguja akiwa na dhamiria ya kuwaunga mkono Vijana ambao wana lengo la kuanzisha mradi mkubwa wa maduka ya biashara na nyumba ya mtumishi.

Makabidhiano hayo yalifanyika Mkoa wa Kaskazini Unguja Mahonda tarehe 09 Disemba, 2023 mbele ya Mwenyekiti wa Mkoa Ndugu Ismail Ali Ussi pamoja na Katibu wa Mkoa na Hamasa wa Mkoa.

Mhe. Munira Mustafa Khatibu ameahidi kushirikiana na vijana wa Mkoa huo ili kuhakikisha vijana wa Mkoa huo kila wanapokuwa na changamoto katika shughuli zao za kuimarisha Jumuiya atahakikisha kuwa nao pamoja nyakati zote zile katika kipindi chake cha uongozi Kama ilivyo kipindi chake kilichopita kuwasaidia vitu mbalimbali vya kiofisi pamoja na Pikipiki ya Jumuiya hiyo.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-12-11 at 00.21.13.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-11 at 00.21.13.jpeg
    75.3 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-12-11 at 00.21.14.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-11 at 00.21.14.jpeg
    78.6 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2023-12-11 at 13.13.36.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-11 at 13.13.36.jpeg
    112.3 KB · Views: 6
Back
Top Bottom