Mbunge Mkenge ashiriki kikao cha umoja wa wazazi, kata ya Kerege

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
1,060
708
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Mhe. Muharami Mkenge ameshiriki Kikao cha Umoja wa Wazazi, Kata ya Kerege.

Mbunge Mkenge amewasihi Viongozi hao kutoa elimu kuhusiana na Malezi Kwa watoto na Vijana maana ndio nguvu kazi ya Taifa.

Pia, Mbunge Mkenge katika Baraza la Wazazi amehaidi kuwapa kadi za Uanachama Umoja wa Wazazi mia tano (500).

Kikao hiko kimeendesha harambee ya Keki yenye lengo la kuchangisha pesa kwa Ajili ya Ujenzi wa Ofisi ya Umoja wa Wazazi Kata ya Kerege na Mbunge Mkenge ametoa ahadi ya Kuchangia Matofali elfu moja (1000). Jumla Kuu ya Kiasi kilichopatikana katika harambee hiyo ni kiasi cha pesa Tsh. Milioni moja, Laki saba na Elfu sabini.

IMG_20230812_210256_446.jpg
 
Back
Top Bottom