Tetesi: Mbunge machachari kutikisa siasa za Tanzania na kumwaga manyanga kabla ya Julai 24

Status
Not open for further replies.

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,829
43,277
Wasalaam wana jamvi!

Niendelee kuwatakia sikukuu njema ya amani na furaha miongoni mwenu!

Wana jamvi kama mtakumbuka siasa za tanzania zilitikiswa mwaka jana kama mara tatu hivi
Mara ya kwanza ilikuwa ni mtuhumiwa wa ufisadi kuhami upande mwingine..wengi hawakutegemea kama atapokelewa.

Mara ya pili ilikuwa kwa nguli wa siasa na Mzalendo Dr Slaa kumwaga manyanga chanzo ikiwa ni kupinga ujio wa mtuhumiwa wa ufisadi kwenye chama chao na hakuwa tayari kushiriki dhambi ya kumsafisha!

Tatu ilikuwa ni pale Prof Msomi na nguli wa uchumi alipo kataa kushiriki dhambi ya kumsafisha mtuhumiwa wa ufisadi na kuamua kumwaga manyanga!

Sasa kabla ya tarehe 24 nchi itatekwa tena na taharuki ya aina yake baada ya mbunge kijana na machachari kuvunja ukimya na kuamua kumwaga manyanga!
Taarifa zinasema mbunge huyo amekuwa kimya kwa kipindi kirefu sana na amekuwa akizushiwa anaumwa ili ionekane hiyo ni sababu kuu!

Hata hivyo amekuwa akipata wakati mgumu sana hasa pale anapo lazimishwa kutoa matamko ili ionekane yupo pamoja nao na amekuwa akikataa na kusema sitaki kuongea na kusema fulani aongee..

Jambo hili limekuwa likiwatesa sana watu wake ndani ya umoja wao na chama chao kwani ukimya wake umekuwa ukizua maswali mengi na wamejaribu kila mbinu za kumlazimisha aongee lakini wameshindwa!

Jambo la kumlazimisha aongee limekuwa likimkera sana na amekuwa akiwa sisitiza kuwa yeye amechagua kunyamaza wasi mlazimishe!

Kibaya zaidi kuna mpango wa kumlazimisha kuongea kwenye mkutano fulani tarehe 24 ambao bado haujawa confirmed! Lakini baada ya kupata habari kuwa amepangwa kuongea na kusema hataki na wasimlazimishe kwani umoja una watu wengi wa kuongea!

Sasa habari zilizopo ana mpango wa kuongea na ataongea kinacho muumiza kabla ya tarehe 24 na atamwaga manyanga na kuachana na ubunge kabisa na kwenda kusoma nje ya nchi....

Baada ya viongozi wake kupata habari hizo wanahaha kumzuia asiongee huku wakitaka kujua anataka kuongea nini na wanampango wa kuhakikisha aengei chochote na wameshambembeleza sana lakini amesimama kuwa kwenye msimamo wako kuwa ataongea kabla ya tarehe 24!

Zina fanyika kila juhudi za kunusuru tukio hilo kwani wanasema litasambaratisha umoja huo kabisa.

Lakini amesisitiza kuwa hayuko tayari kushiriki siasa za kinafiki kamwe...!

Je watafanikiwa kumzuia?
Ni nani huyo?
Ataendelea kukaa kimya?
Ni kwañini hawataki aongee?

Wana jamvi muda huongea tusubiri!

Karibuni wana jamvi!
 
Ubunge aliomba mwenyewe alipita kwenye kura za maoni akashinda akakesha usiku kuchaa kulinda kuraa akashindaa akatangazwaa akasherehekea! Sasa hata kam! akimwaga manyanga hiyo pia itakua ni maamuzi yake haitatikisa kitu sbbu yeye ndo aliomba kura kwa wananchi so akiamua kuachia ngazi ni yeye sioni nchi kutikisika!
 
TUSUBIRI AKIONGEA HATUJUI ATAONGEA NINI
 
Mbona tarehe 24 mbali sana. Abwage tu manyanga sasa sio kutuweka suspense,..wengine wana matatizo ya moyo kusubirini shida.
 
Ndiyo maana pesa imeadimika mtaani. Hili hata Raia Namba Moja wa Tanzania, analijua. Kwa sasa mtaani pesa hakuna...
 
Mbona tarehe 24 mbali sana. Amwage tu manyanga sasa sio kutuweka suspense,..wengine wana matatizo ya moyo kusubirini shida.
Sasa tusimpangie muda na tarehe ya kuongea hii ni nchi ya demokrasia!
 
Kuongea ni haki yake ya msingi na maamuzi yake tutayaheshimu.
Siasa ni mfumo wa maisha kama maisha mengine.
Hivyo sio kwamba ukiwa mwanasia inakuwa kitu cha ajabu kubadilisha fani.
Mbona watu wanahama au kubadilisha kazi hushangai .
Mbona mama Anna Mghwira ameacha siasa na kuamua kwenda kupiga injili.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…