Mbunge Lucy Sabu Katika Ziara ya UWT Taifa Mkoa wa Simiyu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,584
1,189

MBUNGE LUCY SABU NA USHIRIKI WA ZIARA YA UONGOZI WA UWT TAIFA MKOA WA SIMIYU

Mbunge wa Viti Maalum (Vijana Taifa) Mkoa wa Simiyu, Mhe. Lucy John Sabu ameshiriki katika ziara ya viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025.

Ziara ya uongozi wa UWT Taifa Mkoa wa Simiyu imehusisha Mwenyekiti UWT Taifa, Ndugu Mary Pius Chatanda; Makamu Mwenyekiti UWT Taifa, Ndugu Zainab Shomari; Viongozi wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa; Viongozi wa Chama, UWT na Serikali na Mbunge wa Viti Maalum (Vijana Taifa), Mhe. Lucy John Sabu.

"Nimepata fursa ya kuambatana na Makamu Mwenyekiti UWT Taifa, Ndg. Zainab Shomari kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa vitendo katika miradi ya Ujenzi wa Madarasa na Miradi ya Maji katika Kata ya Sukuma na Kata ya Masela na kushiriki Mikutano ya hadhara katika Wilaya ya Maswa, Simiyu" - Mbunge wa Viti Maalum (Vijana Taifa), Mhe. Lucy John Sabu.

"Meatu, Simiyu. Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Zainab Shomari pamoja nami tumetembelea na kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Wilayani Meatu, Simiyu, mradi huo wenye gharama ya Shilingi Bilioni 1.4. Tunaipongeza Serikali kwa kutenga fedha hiyo kwa ajili ya mafunzo ya ujuzi kwa vitendo" - Mbunge wa Viti Maalum (Vijana Taifa), Mhe. Lucy John Sabu.

#UWT IMARA, JESHI LA MAMA
#KAZI IENDELEE
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-09-22 at 13.17.40.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-22 at 13.17.40.jpeg
    58.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-09-22 at 13.17.41.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-22 at 13.17.41.jpeg
    66.7 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-09-22 at 13.17.43.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-22 at 13.17.43.jpeg
    51.8 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-22 at 13.17.44(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-22 at 13.17.44(2).jpeg
    59.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-09-22 at 13.17.44(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-22 at 13.17.44(1).jpeg
    75.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-22 at 13.17.43(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-22 at 13.17.43(2).jpeg
    59.3 KB · Views: 2

Similar Discussions

Back
Top Bottom