Mbunge Lucy Mayenga awawezesha Mama lishe majiko ya gesi Mkoa wa Shinyanga

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,807
1,293
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga ameendelea kuwafikia Wajasiriamali Mkoani Shinyanga ambapo leo ilikuwa zamu ya Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga kupatiwa msaada wa Majiko ya Gesi 165 yenye thamani ya Shilingi Milioni 8.2 kwa ajili ya kuwarahisishia kazi katika shughuli zao na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa utunzaji mazingira kwa kutumia nishati mbadala.

Akizungumza wakati wa kukabidhi majiko 165 yakiwa yamejazwa gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Julai 7,2023 katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Mayenga amesema lengo lake ni kuwafikia akina mama wajasiriamali 800 katika wilaya zote za mkoa wa Shinyanga.

"Tayari nimetoa majiko 250 kwa Mama Lishe Wilayani Kahama yenye thamani ya shilingi Milioni 12.5 , na Majiko ya Gesi kwa Mama Lishe 165 Shinyanga Mjini yenye thamani ya shilingi Milioni 8.25 na nitaendelea kutoa majiko ya gesi katika wilaya zote za Mkoa wa Shinyanga lengo ni kuwafikia wanawake 800 kwa kuwapatia majiko ya gesi" - Mhe. Lucy Mayenga, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga

“Wajasiriamali hawa, mama lishe hawa nimewatafuta kwenye maeneo yao ya kazi bila kuangalia hawa ni wanachama wa CCM ama la kwani lengo langu ni kuona wanawake wanapata furaha. Hii ni sehemu ya kuonesha upendo kwa Wajasiriamali na Mama Lishe pamoja kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wanawake katika shughuli za kiuchumi na utunzaji mazingira kwa kutumia nishati mbadala sambamba kuwapunguzia gharama za kununua mkaa na nishati zingine" - Mhe. Lucy Mayenga, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga

"Nitaendelea kutoa majiko ya gesi 800 mkoa mzima. Majiko haya tayari yana gesi, nina dhamira ya kutoa kwa wananchi kile ninachokipata. Mambo mengine tunafanya kwa sababu ya utashi wetu binafsi lakini pia mambo anayohamasisha Mhe. Rais Dkt. Samia viongozi tufanye katika kuwaletea maendeleo wananchi. Mhe. Rais Samia anataka wabunge tufanye kazi ya kusaidia wananchi" - Mhe. Lucy Mayenga, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga

2C0A2706.jpg
2C0A2870.jpg
F0eM5_yX0AErUmu.jpg
F0eM5_sWYAIyemI.jpg
 
Back
Top Bottom