Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,524
- 1,173
MBUNGE KWAGILWA REUBEN NHAMANILO AZUNGUMZIA UPOTEVU WA FEDHA ZA MADAWA MSD NA WASHITIRI
Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya Bungeni jijini Dodoma amesisitiza kuwa kuna upotevu mkubwa wa fedha za dawa na vifaa tiba kupitia Washitiri. Ashauri maboresho yafanyike.
"Serikali ya CCM imefanya Mapinduzi makubwa kwenye eneo la Afya. Miundombinu ikiwemo vituo vya afya, Zahanati, Hospitali za Rufaa (Mkoa), Hospitali za Kanda. Wajibu wetu ni kuishauri Serikali namna ya kutatua changamoto ili mafanikio tuliyoyapata yasigeuke kuwa laana" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge Handeni Mjini
"MSD kuna miradi minne ya kununua dawa; (1). Ununuzi wa vifaa na vifaa tiba vya huduma ya dharura. (2). Mapambano dhidi ya UVIKO-19. (3). Utekelezaji wa mradi wa Mfuko wa Dunia. (4). Fedha zinazolipwa kutoka kwenye Halmashauri zetu" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo
"Fedha zinazolipwa kutoka kwenye Halmashauri zetu; Hospitali zetu zinapoweka Oder kununua dawa MSD uzoefu unaonesha kwamba uki order dawa kumi MSD wanapata dawa nne, dawa sita hawazipati. Waki order dawa 100 MSD wanapata dawa 40, dawa 60 hawazipati" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo
"Dawa ikikosekana muongozo unawataka Hospitali kununua dawa kwa Washitiri. Washitiri ni tatizo. Handeni Mjini mwaka 2021-2022 MSD tulinunua dawa za Milioni 40 lakini kwa Washitiri tulipeleka Milioni 60. Mwaka 2022-2023 MSD tulipeleka Milioni 55 lakini kwa Washitiri tulipeleka Milioni 61 za kununua dawa" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo
"Fedha zetu nyingi za dawa zinakwenda kwa Washitiri. Tusipopaboresha kwenye mfumo wa Washitiri tatizo la ukosefu wa dawa tutaendelea kuwa nalo. Bei wanayotuuzia Washitiri ni kubwa kuliko ambayo tungenunua MSD" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo
"Washitiri bei wanazotuuzia ni kubwa kuliko Wholesaler Tanzania. Ukiagiza kufaa tiba kinaweza kumaliza mpaka mwaka hakijaletwa. Tuondokaneni na Habari za Washitiri. Washitiri wakiwa wengi waruhusuni wawe na ushindani kwenye" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo
"Bajeti ambayo MSD wanahitaji ni Bilioni 592. Miezi sita iliyopita MSD wamefanya manunuzi ya Bilioni 257. Dawa zinazonunuliwa na MSD na dawa zinazonunuliwa Halmashauri zikisimamiwa vizuri dawa zinatosha. Kinachofanyika tunanunua dawa mara tatu ya bei halisi. Tukafanye Mapinduzi kwa Washitiri." - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo
"Dawa inapoagizwa ikachelewa kuja kwa miezi tisa kwa mwaka, huu ni umasikini mkubwa. Magari yanaweza kuja Dar es Salaam yakakaa kwenye bonded housewares, inashindikana nini tukawa na bonded housewares za madawa?" - Kwagilwa Reuben Nhamanilo
"Wizara ya Afya katika eneo mnalotakiwa mliboreshe ni namna maoteo ya dawa yanavyofanyika, haya ndiyo yanapelekea dawa zichomwe. Tunaagiza zaidi ya tunavyotumia. Kinachofanyika ni matumizi mabaya ya usimamizi. Kwanini tusiwe na bonded housewares za madawa na vifaa tiba?" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo
"Mzalishaji akizalisha dawa Urusi aje ahifadhi hapa Tanzania. Akizalisha Ujerumani aje ahifadhi hapa Tanzania ili MSD akihitaji dawa saa mbili asubuhi saa saba mchana dawa zimeshafika. Nini kinashindikana? - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo.