ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 61,759
- 72,193
Hongera sana Mbunge Kunambi Kwa kuwasemea na kuwatetea Watumishi.
Sio tuu kwamba wadogo Wanaonewa Bali wanachomekwa kwenye madudu ya wakubwa kuwalinda hao wakubwa Wala rushwa.
Amazingira haya nimewahi yashubudia mara nyingi sana.
TAKUKURU ni taasisi ambayo inatumika kuwakandamiza Watumishi wadogo wa Umma lakini ni nadra sana kuja kusikia imemkamata Mkuu wa taasisi au mwanasiasa.
---
Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi, ametoa rai ya kulenga uwajibikaji kwa viongozi wa juu kama njia ya kudhibiti tatizo la rushwa katika taasisi za umma.
Akizungumza bungeni jijini Dodoma, Oktoba 29, 2024, Kunambi ameeleza kuwa utamaduni wa utawala hujengwa na viongozi wa juu wa taasisi, na hivyo tatizo la rushwa huanzia kwa viongozi hao badala ya watumishi wa ngazi za chini.
“Kuna kitu kinachoitwa utamaduni wa utawala. Kitu hiki kinajengwa na kiongozi wa taasisi,” amesema Kunambi, akiongeza kuwa kushughulikia wafanyakazi wa ngazi ya chini pekee bila kuwawajibisha wakuu wa taasisi hakutakuwa na athari kubwa katika kudhibiti rushwa.
Amesisitiza kwamba, badala ya hatua kuchukuliwa dhidi ya watumishi wa kawaida, sheria na uwajibikaji vikielekezwa kwa wakurugenzi na viongozi wa juu itaweza kusaidia kuondoa mazingira yanayoruhusu rushwa.
Akiendelea, Kunambi amehimiza viongozi wa juu kubeba jukumu la kujenga na kudumisha maadili bora ya utawala ili kupunguza changamoto za rushwa zinazoathiri taifa.