BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 367
- 434
Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora amewakumbusha viongozi na CCM -Halmashauri ya Chalinze kuwapa kipaumbele Mabalozi katika kazi za kila siku zinazofanywa na fursa zinazojitokeza ili kuwatambulishaU umuhimu wao katika kazi na ustawi wa Chama.
Maneno hayo ameyasema alipokuwa akiongea na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kata ya Msoga kwenye mkutano Mkuu maalum wa kupokea taarifa ya miaka Mitatu ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kata hiyo.
Katika kikao hicho ambapo pamoja na kupokea Ilani, Ndg. Mbunge aliwagaia Mabalozi 180 wa Kata ya Msoga kadi za Bima ya Afya kwa ajili ya kupata huduma ya afya pale inapotokea hitaji la matibabu, aliwaasa kutambua umuhimu wao na kuwaasa kuwa haya yanayofanyika ni kwa ajili ya kuwaimarisha wakitumikie Chama Chao na kuwa Chama kinawajali.
Akimshukuru Mbunge wa jimbo hilo, Diwani wa kata ya Msoga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze alimuhakikishia Mbunge kuwa Chalinze ususani kata hiyo itqendelea kuwa ngome ya CCM na kwamba wamejipanga kwa ajili ya ushindi katika chaguzi zote mbili wakianza na hii ya Serikali ya Mtaa 2024 na baadae ule Mkuu wa 2025.
#KaziInaendelea #MikutanoMrejesho