Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,584
- 1,189
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza amefanya Ziara ya Kata kwa Kata huku akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa Kata ya Harungu iliyopo Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.
Akiwa katika Kata ya Harungu, Mhe. Juliana Daniel Shonza amekabidhi mifuko ya Saruji 20 yenye thamani ya Shilingi Laki Nne (400,000) kwaajili ya Ujenzi wa Ofisi ya Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Kata ya Harungu.
Mhe. Juliana Daniel Shonza ameelezea Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025; Kuzungumza na Wanawake kuhusu utolewaji wa mikopo ya Asilimia Kumi (10%); Kuwezesha Wanawake Wajasiriamali Kiuchumi; Kuendesha Kampeni ya Kupinga Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia; Kuendesha Kampeni ya Kupinga Mimba za Utotoni; Kampeni ya Kuhamasisha Lishe Bora kwa Mama na Mtoto.
Mhe. Juliana Daniel Shonza amesisitiza sana Wananchi wote wa Kata ya Harungu kujitokeza kwa wingi Kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ili wapate haki ya kupiga kura wakati wa uchaguzi.
Mwisho, Mhe. Juliana Daniel Shonza amewasihi wananchi wote na viongozi kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri sana aliyofanya nchini ikiwemo Mkoa wa Songwe.