Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,588
- 1,190
MBUNGE JANEJELLY ACHANGIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA, MUONE HAPA
Mbunge wa Viti Maalumu, Anayewakilisha Wafanyakazi Nchini, Mhe. Janejelly James Ntate ameunga mkono hoja na maoni ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda huku akisema kuwa hayo yametokana na kazi aliyoifanya Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Wizara hiyo ikiwemo kufufua viwanda vingi vilivyokufa nchini.
Mhe. Janejelly James Ntate amevitaja viwanda hivyo kuwa ni pamoja na kiwanda cha Kilimanjaro Tools kilichofungwa kwa miaka 34, kiwanda cha TEMDO, CAMARTEC na Liganga na Mchuchuma ambapo viwanda vyote hivyo vimegharimu serikali mabilioni ya fedha.
Hata hivyo ameishauri serikali kuangalia upya sera za manunuzi kwa kuwa kiwanda cha TEMDO kimekuwa kikikwamishwa kupata tenda za vifaa vya afya Serikalini kwa sababu ndogondogo wakati kazi za kiwanda hicho kimepitishwa na MSD na serikali inatumia pesa nyingi za kigeni kununua vifaa hivyo hivyo nje ya nchi.