Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,618
- 1,198
MHE. JAFARI CHEGE WAMBURA AFANYA ZIARA NA MKUTANO KATIKA KATA YA KITEMBE
Mbunge wa Jimbo la Rorya Mkoa wa Mara, Mhe. Jafari Chege Wambura ameanza ziara rasmi na kufanya Mkutano wa kwanza katika Kata ya Kitembe Wilaya ya Rorya
"Wakati nawaomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Rorya mwaka 2020 niliwaambia naweza nisiwe na fedha za kumgawia kila mwananchi, hata kama ningekuwa nazo bado hiyo siyo kazi ya Mbunge anayetokea kwenye Jimbo masikini, niliwaambia naombeni kura zenu" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Niliwaambia, Mtakaponipa kura kazi yangu kubwa kama Kiongozi ni kutumia akili na maarifa yangu, ushawishi na namna ya kuzungumza, kujenga hoja, kufuatilia mambo mbalimbali ili baada ya Miaka kadhaa tuwaonyeshe watu wa Rorya nini tumefanya" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Kazi kubwa ya Mbunge anayetokea Jimbo la wananchi masikini wanaotaka kujua mustakabali wa Afya maana Afya ni Msingi wa maisha yao, akina Mama wanaojifungua wanajifungua wapi wakiwa salama maana ule ni uhai na ndiyo maisha yao" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Wananchi wanataka wajue wanapataje Maji safi na salama kwenye maeneo yao kwasababu hiyo ndiyo inawaondolea magonjwa nyemelezi ikiwemo Kichocho na magonjwa mengine, na kuondoa ugomvi kati ya Baba na Mama kwanini Maji hakuna nyumbani" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Wananchi wanaotoka maeneo masikini kama Rorya wanataka wajue Mbunge unakwenda kufanya nini barabara zipitike muda wote, Wananchi wasiteseke kwenye maeneo wanayoishi wanapotaka kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo jingine " - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Wananchi wanaotoka maeneo masikini kama Rorya wanataka kujua namna umeme unavyoweza kuwafikia Wananchi kwenye maeneo yote ili waweze kutumia umeme" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya