Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,588
- 1,190
MHE. JACQUELINE KAINJA, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora Aishauri Wizara ya Afya Kuanzisha Kurugenzi ya Famasia (Idara ya Huduma ya Dawa na Vifaa Tiba - Pharmacy).
"Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuanzia 23 Julai 2023 mpaka Machi 2024 Idara ya Famasi imeingiza Shilingi Bilioni 34. Lakini kuna Idara zimetengenezewa Kurugenzi zake kama Idara ya Vipimo, Maabara na Mionzi ambayo imeingiza Shilingi Bilioni 9. Kurugenzi ya Nursing imeingiza Shilingi Bilioni 8. Kurugenzi ya Medical Services imeingiza Shilingi Bilioni 8. Kurugenzi ya Surgical Services imeingiza Shilingi Bilioni 19" - Mhe. Jacqueline Kainja Andrew, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora
"Idara zilizotengenezewa Kurugenzi zimeingiza mapato. Idara ya Famasi ambayo nusu ya bajeti ya Hospitali inaenda Famasi na nusu ya mapato ya Hospitali yanatoka Famasi, kwanini hamuweki Kurugenzi ya Famasi?" - Mhe. Jacqueline Kainja Andrew, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora