Mbunge GODBLESS LEMA akutana uso kwa uso na MAGESA MULONGO

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,973
9,568
Ilikuwa hivi:
Mheshimiwa Lema pamoja na waheshimiwa wabunge wenzake pamoja na uongozi wa chama walikuwa wameingia City Park kwa ajili ya chakula cha mchana.

Ghafla Mkuu wa Mkoa naye akaingia City Park bila kujua kamanda Lema yupo pale. Kuona hivyo ilibidi awasiliane na polisi.

Baada ya muda akaingia RPC, pamoja na viongozi wengine wa usalama kuja kumlinda Magesa Mulongo, wapo polisi wa kutosha. Muda huu yupo mezani amepewa ulinzi wa kutosha chini ya RPC.

Mulongo anajua alitenda dhambi ya makusudi, sasa anaishi kwa mashaka akidhani anaweza kulipiziwa kisasi.
Hii ni ajabu Mkuu wa Mkoa analindwa na uongozi wa juu wa mkoa akiwa mezani pamoja na maaskari wa kumwaga.

Mulongo amani yako umeipoteza mwenyewe.
 
Huyu jamaa bora aondoke Arusha,unless kama siyo kufa kwa pressure bac atakufa...!bora aende kwingine kabisa kwa usalama zaidi!
 
kwahiyo kumbe sasa hivi anaishi kama digi digi maskini mulongo ila hii iwe fundisho na ahame kabisa arusha
 
Mkuu Mungi nawe upo hapo unapata chakula cha mchana na waheshimiwa wabunge? Viongozi wa mkoa wa Arusha (Mbunge na Mkuu wa Mkoa) tumieni hekima katika kuuongoza huo mkoa. Hilo tu

Umeeleweka kiongozi
 
Ilikuwa hivi:
Mheshimiwa Lema pamoja na waheshimiwa wabunge wenzake pamoja na uongozi wa chama walikuwa wameingia City Park kwa ajili ya chakula cha mchana.
Ghafla Mkuu wa Mkoa naye akaingia City Park bila kujua kamanda Lema yupo pale. Kuona hivyo ilibidi awasiliane na polisi.
Baada ya muda akaingia RPC, pamoja na viongozi wengine wa usalama kuja kumlinda Magesa Mulongo, wapo polisi wa kutosha. Muda huu yupo mezani amepewa ulinzi wa kutosha chini ya RPC.

Mulongo anajua alitenda dhambi ya makusudi, sasa anaishi kwa mashaka akidhani anaweza kulipiziwa kisasi.
Hii ni ajabu Mkuu wa Mkoa analindwa na uongozi wa juu wa mkoa akiwa mezani pamoja na maaskari wa kumwaga.

Mulongo amani yako umeipoteza mwenyewe.......................
Sasa akishapoteza nafasi ya mkuu wa mkoa, atalindwa na nani?
 
haya ndio mambo ya movie za kihindi, wewe ulikuwa meza moja na RC mpaka umesikia anamwita RPC?
 
Lema naye awaite makamanda kwa ajili ya kuzomea hadi ugali umkabe. Kama ni mwanaume na si Mkameroni basi ajilinde mwenyewe anawaita Polisi wa nini. Kalianzisha ngoma basi alicheze
 
Back
Top Bottom