LGE2024 Mbunge Gekul: Tuwalipe CCM kwa kura nyingi kesho

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,274
3,562
Wakuu,

Tunawalipa CCM kwani wanatudai nini?

====

Screenshot_20241126_203724_Instagram.jpg

Mbunge wa Jimbo la Babati mjini Mhe. Paulina Gekul amewataka Wananchi wa Jimbo hilo kuhakikisha wanarudisha shukrani kwa Chama cha Mapinduzi kwa kukipa kura nyingi za ushindi kesho Jumatano Novemba 27.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa:
LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Amewaambia Wananchi kuwa hawapaswi kupeleka kura hata moja kwa upinzani kwa kuwa Maendeleo yote yaliyopo kwenye mitaa yao yamefanywa na Chama cha Mapinduzi chini ya mwenyekiti na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan akisaidiwa na madiwani na mbunge.

“Yaani niwambie ukweli kama ni upinzani ni mimi nilikuwa mpinzani haswa lakini kwa kazi kubwa inayofanywa na serikali ya chama cha Mapinduzi,sioni haja ya kuwa kwa vyama hivyo”

Amesema kwa chama cha Mapinduzi iwe jua au unyeshe mvua ushindi ni mapema kwa kuwa Wana kitu cha kuwaeleza Wananchi.

Gekul amewanadi wagombea wa Chama cha Mapinduzi Mtaa wa Nyunguu, Sawe Sigino na Nakwa.

Kwa Upande wake mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mjini Babati Elizabeth Marley amewataka Wanaccm wajitokeze kwa wingi kupiga kura mapema kisha warejee nyumbani kusubiri matokeo.

Uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji unafanyika kesho Jumatano Novemba 27,2024.
 
Back
Top Bottom