Mbunge Esther Malleko akichangia Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi a Waziri Mkuu Mwaka 2024-2025 ya Tsh. Bilioni 350.9

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,584
1,189

MHE. ESTHER EDWIN MALLEKO, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Akichangia Bajeti katika Majadiliano ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu Mwaka 2024-2025 ya Tsh. Bilioni 350.9.

"Natoa pongezi za dhati kwa Rais wetu Mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyofanya kazi vizuri ya kutuletea maendeleo. Ninampongeza Waziri Mkuu, Naibu Waziri Mkuu, Mawaziri wa Wizara, Manaibu Mawaziri na watendaji wote wa Ofisi ya Waziri Mkuu" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Nampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya, katika miaka mitatu alisema #KaziIendelee na kweli tunaona #KaziInaendelea" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Tumeona ujenzi wa Reli ya Kati (SGR) KM 1219, Serikali ikiwa imetoa Shilingi Trilioni 10.6. Mradi wa kufua umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) na tayari Megawatts 2115 zinazalishwa katika utekelezaji huo na tayari utekelezaji umefikia asilimia 96.8 katika mitambo 9 mmoja tayari umewashwa na tayari Megawatts 235 zimeingia kwenye Gridi ya Taifa na tatizo la umeme limepunguzwa" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Kilimanjaro

"Uboreshaji wa Shirika la Ndege Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan tayari amelipa kiasi cha Shilingi Bilioni 753. Ndege tatu zilizoagizwa tayari Ndege 2 zimeshafika na moja itafika Aprili 2024 na tutakuwa na Ndege 16 katika Shirika la Ndege Tanzania" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kufanya kazi kubwa, mradi wa ujenzi wa Mafuta Ghafi kutoka Hoima - Uganda 🇺🇬 mpaka Chongoleani - Tanga, Tanzania 🇹🇿 KM 1445 kwa kiasi cha Dollar 268.7. Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi kimekamilika kwa asilimia 99 na Serikali imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 320.5 kiwanda kimeanza kuzalisha na mpaka sasa kimezalisha Tani 1851 inayoenda kupunguza uhaba wa Sukari nchini na imeongeza ajira 1,996" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Katika Mkoa wa Kilimanjaro shughuli za kiuchumi zinazofanyika ni pamoja na Kilimo, Biashara na Utalii. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti kwenye kilimo. Wakinamama na wananchi wa Kilimanjaro wanalima Ndizi, Kahawa na Parachichi" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan kuongeza bajeti kwenye Kilimo, kwapatia Maafisa Ugani Pikipiki bado kuna changamoto zinazowakabili wananchi wetu hasa wanawake wakulima wa Mkoa wa Kilimanjaro. Changamoto mojawapo ni Mbegu bora au miche bora inayopelekea kuwa na mazao yasiyokidhi vigezo na wanakosa faida au thamani kutokana na kile wanacholima" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Nashauri, Maafisa Ugani waweze kuwatembelea wakulima wetu, wafanye utafiti, wajue afya ya udongo na kuwashauri Wakinamama na wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wanaofanya kilimo ili waweze kulima kilimo cha kisasa" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Utegemezi wa Mvua za Msimu, mpaka leo tunategemea Mvua za Msimu, kama Mvua za Msimu hazipo watu hawapati kilimo walichokuwa wanategemea kupata mavuno waliyokuwa wanastahili. Nashauri Serikali ifuatilie kwenye Kilimo cha Umwagiliaji, waweke mabwawa ya kutosha, Mvua zinanyesha zinaleta athari kwa wananchi na wakati mwingine mpaka Mafuriko. Kwanini Serikali isione namna gani ya kuweza kutumia maji kwenda kwenye Kilimo cha Umwagiliaji?" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Elimu kwa wananchi namna gani ya kuongeza thamani ya ubora wa mazao yao. Zao kama la Kahawa, wananchi wanauza Kahawa ghafi na wanauzia nchi ambazo hazina hata mche mmoja wa Kahawa kati nchi yao. Wao wanachofanya ni kwenda kuongeza thamani kidogo tu lakini wanapata faida mara tatu mpaka mara tano ya faida anayopata mkulima anayeteseka tangu anapoanza kupanda mche mpaka anapovuna" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Kilimanjaro

"Soko la ndani na nje, bado tumekuwa na shida kubwa sana ya kupata masoko kwaajili ya bidhaa zetu. Ndizi zetu kinamama wa Kilimanjaro tunataka kuona zinaenda nje ya nchi. Zisiishie kupelekwa Mabibo, kutengeneza Mtori. Ndege za mizigo zilizoletwa zitumike kupeleka mizigo nje ya nchi ili watu wetu wapate faida na fedha za kigeni" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Suala la kutokuwa na takwimu sahihi za idadi ya wakulima. Leo Ukitaka kuwahudumia watu ni lazima ujue idadi yao kama ambavyo nchi inavyotaka kuwahudumia wananchi inafanya Sensa lakini hawajui wakulima wako kiasi gani, wanalima kwa kiasi gani, wana mashamba kiasi gani. Kama tunahitaji Mbolea, Pembejeo Miche, wanawezaje kujua kama hawajui idadi ya wakulima. Serikali iangalie ni namna gani itapata takwimu sahihi za wakulima wa Kahawa, Ndizi, Parachichi na Maua ili kuwapa stahiki zao pale wanakuwa wanahitaji Pembejeo na Mbolea" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro wanataka kusikia Serikali inasema nini juu ya ile fedha inayotoka Halmashauri yaani asilimia 10 (4, 4, 2). Wamekaa wakisubiri kwa muda mrefu, tunajua Serikali inafanya mikakati na Mipango ya kuweza kuboresha lakini basi waweze kupewa taarifa ni lini fedha hiyo inatoka na watoe tamko Serikali ili wakinamama wa Kilimanjaro waweze kufaidika" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro
 

Attachments

  • maxresdefaultXCVFGTR.jpg
    maxresdefaultXCVFGTR.jpg
    104 KB · Views: 1
Back
Top Bottom