Mbunge Atupele Mwakibete ataka benki nchini kuwapa Mikopo wanavijiji kupitia hati za umiliki Ardhi za Kimila

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,584
1,189
"Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya mambo makubwa na kuzidi. Waziri Mkuu ulitembelea Mkoa wa Mbeya ikiwemo Halmashauri ya Busokelo, tunakushukuru sana. Lakini mojawapo ya changamoto nchini kumekuwepo na tatizo la kutolewa kwa hati za ardhi za kimila ambazo hazithaminiwi na Taasisi za kifedha za kibenki hususani wanapokwenda kukopa na wamekuwa wakizungushwa hatimaye wanakata tamaa" - Mhe. Atupele Mwakibete, Mbunge wa Jimbo la Busokelo​

"Wananchi wanaoishi vijijini wameendelea kuwa masikini kwasababu hawapati mikopo kupitia hati za kimila za ardhi. Tatizo limetokana na sheria namba tano ya mwaka 1999 inayotoa hati hizi. Je, ni mkakati gani wa Serikali ili kuwarahisishia wananchi wa vijijini waweze kupata hati kama wanavyopata mijini na ziweze kuthaminiwa na benki kwa kubadilisha Sheria namba tano ya mwaka 1999?" - Mhe. Atupele Mwakibete, Mbunge wa Jimbo la Busokelo

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Taasisi za fedha Nchini kuzitambua hati za kimila kama dhamana ya kutoa mikopo kwa Wananchi.

Amesema kuwa hati zote zinazotolewa na Wizara au za kimila zinatambulika kisheria na zina fursa kwa mwenye hati hiyo kupata mikopo kutoka kwenye Taasisi za kifedha.

Ametoa wito huo Bungeni Alhamisi, May 30, 2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa Busokelo, Atupele Mwakibete kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu ambaye alitaka kujua ni lini Serikali itabadili Sheria ya Ardhi ili Watu wa vijijini watumie hati za kimila kupata mikopo.

Amesema kuwa inawezekana zipo Taasisi za kifedha ambazo hazikubali hati hizo kwasababu ya matakwa au mpango kazi wao lakini kwa mujibu wa Sheria hati hizo ni halali na zinatolewa kisheria kwa vipindi kama ilivyo zile zinazotolewa na Wizara kwa miaka 33, 66 hata 99

“Nitoe wito kwa Taasisi zote za kifedha ambazo zimeridhiwa na Serikali kufanya shughuli zake Nchini kwa mujibu wa Sheria za Nchi ziendelee kutumia na kutoa fursa kwa wenye hati za kimila au zinazotolewa na Wizara ya Ardhi kuwa ni hati halali zinatambulika na zinatoa fursa kwa mtanzania anayemiliki ardhi nchini kupata mkopo”
 
Back
Top Bottom