Mbunge ataka wanaotiwa hatiani kwa kosa la ubakaji waondolewe Uume

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,487
3,568
Hoja ya adhabu kwa wanaobaka watoto chini ya miaka 10, imeibuka bungeni mmoja wa Wabunge akitaka wanaotiwa hatia waondolewe uume.

Mbunge wa Viti Maalumu, Rita Kabati amesema hayo leo Jumatano Septemba 4, 2024 wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma.

Mbunge Kabati amesema ubakaji umeshika kasi hasa katika Mkoa wa Iringa ambako imetokea kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 18, kubakana wenyewe kwa wenyewe.

“Je sheria inasemaje kwa vijana wanaobakana wenyewe kwa wenyewe kwenye shule huko? Lakini pia hili tatizo limekuwa ni kubwa sana hapa nchini na tumeona hadi wauawe?” amehoji.

Amesema yeye anaona wanaokutwa na hatia kwa makosa hayo watolewe uume maana ndiyo umekuwa tatizo kubwa.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Jumanne Sajini amesema
amesema kutokana na mmomonyoko wa maadili, baadhi ya matukio ambayo hayakuzoeleka kusikika awali, yameongezeka kwa kasi ikiwamo ubakaji.

“Na sasa amesema kwa watoto ipo mashuleni, kosa hata kama limefanywa na mtoto ni kosa lakini kwa maana sheria zetu mtoto atahukumiwa kwa mujibu wa sheria za watoto,” amesema.

Amesema ikitokea mtoto amemfanyia mwenziwe vitendo vya uvunjifu wa maadili kama hivyo na taarifa zikitolewa katika vyombo vya dola, kisha kupelekwa mahakamani mtoto atahukumiwa kwa mujibu wa sheria.

Amesema ikiwa kama atahukumiwa kifungo basi atafungwa katika Mahakama za watoto.

Kuhusu kuondolewa uume, Sajini amesema ni kweli jambo hilo linaudhi lakini hicho anachokisema hakipo katika sheria za nchi.

“Kama tutafika hatua hiyo ni pale ambapo Bunge litakuwa limebadilisha sheria na kuruhusu alichosema mbunge,” amesema.
 
Back
Top Bottom