Mbunge Assa Makanika: Kigoma Kuunganishwa kwenye Grid ya Taifa kwa Njia Sita za Umeme

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,296
1,100

MBUNGE ASSA MAKANIKA ATOA MSISITIZO KWA MABALOZI KUHAKIKISHA WATU WANAJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Mhe. Assa Makanika akiwa katika ziara yake ya kuzungumza na Mabalozi wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo lengo ikiwa ni kuhamasisha na kuwahimize watu kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ikiwa ni pamoja na kuwapatia vitendea kazi (T-Shirt, bendera) Mabalozi wote wa Chama cha Mapinduzi.

"Mabalozi hakikisheni watu wajitokeze waende wakajiandikishe kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura. Ushindi tunaosema tuna Mbunge wa CCM umetokana kwasababu watu walijiandikisha, ili tupate Diwani anayetokana na Chama Cha Mapinduzi hakikisheni wanachama wanaenda Kujiandikisha" - Mhe. Assa Makanika, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini

"Sisi Wabunge wa Mkoa wa Kigoma tukamuona Mheshimiwa Makamu wa Rais ambaye naye alifikisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alikuja Kigoma kwasababu anaipenda Kigoma"

"Umeme katika Mkoa wa Kigoma tuna njia Sita zitakazoiunganisha Kigoma katika Gridi ya Taifa ambazo ni Nyakanazi - Kibondo (Kilovolt 33) Majenereta ya Kibondo yameshazimwa. Njia zilizobaki zitaunganisha Kigoma, Uvinza. Kigoma tuna njia ya umeme yenye msongo wa Kilovolt 400 itashuka kutoka Nyakanazi mpaka Kidahwe. Njia ya Kilovolt 33 kutoka Tabora, Uvinza mpaka kitovu kikuu cha kupokea umeme wote Mkoa wa Kigoma" - Mhe. Assa Makanika, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-07-13 at 23.52.32.mp4
    24.8 MB
Back
Top Bottom