figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Uchawi hasa kwa Vijana haujawahi kumuachaga mtu Salama asilani...!!!!!!!Mbunge wa Mkuranga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdallah Ulega amewafananisha wabunge wa upinzani na popo kuwa hawaeleweki na kusema wamekuwa watetezi wa wawekezaji ambao wao wamewatuhumu kuwa ni wezi wa madini.
Mbunge huyo amesema hayo jana bungeni akisema kuwa wapinzani hao leo limewashuka baada ya jana Rais Magufuli kukutana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton na kukubaliana kuwa kampuni hiyo ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.
“Popo hajafahamika kama ni mnyama au ndege mpaka hivi leo na hawa wenzetu hata sitaki kuwaita vinyonga naomba niwaite popo maanake hawajafahamika kama ndege au wanyama na leo limewashuka kwani walijigeuza kuwa mawakili mwa wale ambao sisi tunawatuhumu kwamba ni wezi wetu na yule anayehusika Mkuu amewathibitishia mchana wa leo (jana) ameingia na amekiri mwenyewe kwa kinywa chake ya kwamba wapo tayari kulipa pesa ambazo tunazowadai na tena lile lililokuwa linaonekana jambo gumu la kujenga kinu cha kuchenjua madini amelichukua na amesema yupo tayari kujenga” alisema Ulega
Mbunge huyo alikwenda mbali zaidi na bara la Afrika limekuwa na bahati mbaya kwani wapinzani wa Afrika wamekuwa wakitumika na mabeberu miaka yote na kusema wao kama Chama Cha Mapinduzi wanakila sababu ya kutamba kwa kuwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM imeweka sawa na kutamka namna nzuri ya kusimamia shughuli za madini.
Ulizaliwa kwa bahati mbaya huna tofauti na akili za mtoto aliyepatikana kwa mganga wa kienyeji,Tatizo lako umeamua kuweka akili yake mfukoni na kuanza kuvuja povuTunampongeza kwa Kusema Ukweli!
Tunampongeza kwa Kusema Ukweli!
Chadema ni mbadala wa shetani hapa Tanzania
Ujinga huonyeshwa kwenye kauliwabunge wote tu hawaeleweki sio wa upinzani tu. hizi siasa nazo!!!!
Tatizo la popo huwa hawasikii ingawa wana masikioNimemsikiliza kwa makini. Nimesikitika kupoteza muda wangu kumsikiliza. Ni upupu mtupu. Hajielewi. Mbaya zaidi amejidhalilisha kwa dume zima lililovaa suti kuongea kikicheni pati huku akitingisha mwili kama demu. Ndugu zake wanauawa hovyo huko pwani wakati yeye anamwaga ushuuzi bungeni. Yaani hovyoo kabisa. Tunahitaji sasa wabunge walio na upeo mkubwa zaidi ya kujua kusoma na kuandika mithili ya huyu mwanaume suruali!
Mbona umeishia kutoa povu tu bila kujenga hoja na kumpinga kwa hoja? Mleta post amejenga hoja kwa kutoa mifano iliyo halisi lakini wewe umeishia kukashifu tu.Nimemsikiliza kwa makini. Nimesikitika kupoteza muda wangu kumsikiliza. Ni upupu mtupu. Hajielewi. Mbaya zaidi amejidhalilisha kwa dume zima lililovaa suti kuongea kikicheni pati huku akitingisha mwili kama demu. Ndugu zake wanauawa hovyo huko pwani wakati yeye anamwaga ushuuzi bungeni. Yaani hovyoo kabisa. Tunahitaji sasa wabunge walio na upeo mkubwa zaidi ya kujua kusoma na kuandika mithili ya huyu mwanaume suruali!