Nimekuwa nikisikia mara kadhaa kuwa mbu akimng'ata binadamu basi mbu huyo anakufa hapo? imekaaje hii wakuu?
- Tunachokijua
- Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika tovuti ya taifa ya dawa ya nchini Marekani kuna aina zaidi ya 3,500 za mbu kutoka katika mabara tofauti isipokuwa Antarctica. Katika aina zote hizo za mbu ni aina chache tu za mbu ambao wanaweza kuambukiza magonjwa kwa bidanadamu ikiwemo Malaria.
Mbu jike anaweza kuishi hadi miezi mitatu na zaidi kulingana na aina husika ya mbu na anaweza kutaga hadi mayai 300, mbu hula sukari inayopatikana katika maua. Mbu jike hutumia mate yake anapokuwa ananyonya damu ili kuitenga damu na maji na kusaidia damu hiyo kutoganda anapokuwa anafanya zoezi hilo. Mate ambayo hupelekea muwasho kwa aliyen’gatwa.
Ukweli upoje?
JamiiCheck imepitia tafiti na machapisho mbalimbali ili kubaini uhalisi kuhusu hoja hiyo na kubaini kuwa hoja hiyo si ya ukweli. JamiiCheck imebaini kuwa ni mbu jike pekee ndiye anayemuuma binadamu na wanyama wengine ili aweze kupata damu itakayomuwezesha kuyapa rutuba mayai yake kwa kuyaongezea protini na asidi za amino.