Mbowe na Lissu wawasili Arusha kumtembelea Lema

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,279
Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe.Freeman Mbowe akiwa Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu wamewasili Arusha Tayari kwenda kumtembelea Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe.Godbless Lema aliyeko Magereza Kisongo.
PICHANI Katibu wa Kanda
ya Kaskazini akitoa Mwongozo.
Baada ya kutembelea Mbunge Godbless Jonathan Lema Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe pamoja na Mwanasheria huyo Tundu Lissu wataongea na vyombo vya habari .

===========
Muda huu Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe.Freeman Mbowe pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Chadema Mhe.Tundu Lissu wapo Magereza wanazungumza na Mbunge wa Arusha Mjini.
Katika msafara huo Mwenyekiti Ameongozana Mhe.Ester Bulaya Mbunge John Mrema Pamoja na Katibu wa Kanda ya Kaskazini Mhe.Amani Golugwa.
John Mrema.
Nimemtembelea Lema Leo tare he 13.01.2017 katika gereza la kisongo nikiwa nimeambatana na Mh.Mbowe,Lissu na Ester Bulaya.

Nimefarijika kumkuta akiwa na moyo Mkuu na ametuma ujumbe kuwa tusikatishwe Tamaa bali tuongeze kasi ya Mapambano ya kudai haki


 
Nakumbuka msemo wa Lema kwamba dhambi kubwa kuliko zote duniani ni Uoga.
Anaonyesha wapigakura wake kwa vitendo jinsi asivyo Mwoga.
Godbless Jonathan Lema Mungu ampe maisha marefu ni mbunge ambaye siku zotr husimamia anachokiamini hujawahi kurudi nyuma katika mapambano ya kupigania haki.
Yaani Leo ndo wamemkumbuka! Daaah inasikitisha.
Nakumbuka msemo wa Lema kwamba dhambi kubwa kuliko zote duniani ni Uoga.
Anaonyesha wapigakura wake kwa vitendo jinsi asivyo Mwoga.
 
Lile Branch la Chama Tawala halijatuma Defenda kuwazuia hao Makamanda ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…