Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,857
- 4,866
Wakuu,
Mbowe atoa neno baada ya Lissu kutangazwa kuwa Mwenyekiti Mpya Taifa, anza kwa kushukuru Mungu kwa zoezi zima kwenda vizuri bila ya kuwa na changamoto yoyote na kujenga chama chenye heshima, hadhi, maono, chama kilichojaa matumaini ya wote wanaoitamani kesho iliyobora zaidi.
Mbowe asema aliahidi kuwa watafanya uchaguzi wa kihistoria, sasa dunia imeona wenyewe, kuwa kile kalichoahidi wamekitenda.
Mbowe amewashukuru Lissu pamoja na Makamu wake Heche kwa ushiriki wao, asema anapomkabidhi vijiti vya kuiongoza CHADEMA
Pia soma: Pre GE2025 - Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%
Wamefanya uchaguzi huru na haki ambao kila mtu ameona, lakini uchaguzi ni mchakato, na hili halipaswi kuwa tukio la siku mmoja, inatakiwa kuwa mchakato wote unaojengwa hadi siku ya mwisho.
Kwa namna ambavyo wagombea na mashabiki wao walifanya kampeni na wapambe wao umeacha maumuvu na majera makubwa makubwa ambayo yameumiza wengi na yanapaswa kuponywa ili kutoharibu brand ya CHADEMA
Ushauri wake kwao ni kuwa waende kuponya chama. Anasema moja ya mambo aliyoahidi kufanya kama angepewa nafasi ya kuwa Mwenyekiti kwa mara nyingine ni kuunda Tume ya Ukweli na Upatanishi, ili watu wakazungumze kuhusu maumuvu yaliyotokea ili wote wakaongee, kupatana na kuponya maumivi.
Mbowe asema awaasa kama baba wa chama, ila akaongeza kuwa anawaagiza kuunda tume ya ukweli naupatanishi kutibu majeraha ili waweze kujenga umoja. Asema kuwa alisema ulishindi wa yeyote ni ushindi wa chama, kusiwe na yeyote atakayefanya kiburi bali wafanye kazi kwa umoja na kujenga chama.
Asema wasitembee kwa mawazo yao binafsi bali watumie katiba yao, na pale wanapoona kuna upungufu kwenye katiba washirikiane na wengine katika kutafuta suluhu.
Mbowe amalizia kwa kusema anaondoka CHADEMA akiwa anajivunia sana kwa kazi aliyoifanya kwa zaidi ya miaka 30